Ads (728x90)

Kilo chako ndicho, hicho sitarijie kisicho,
Katu sikodoe macho,ukadhani ndicho hicho,
Kwa macho utamanicho, kitakutoboa macho,
Epuka njia za chocho,si maisha pochopocho.

Wakatabahu.

Post a Comment

  1. Nilidhani ni mpweke, katika fani ya peke, ambayo kwayo ipweke watumiao wachache,

    ReplyDelete
  2. watumiao wachache
    hao wengi waache
    ushairi kwao kasheshe
    kwangu mimi ni cheche

    ReplyDelete
  3. UGENINI AU NYUMBANI
    MJINI AU NYIKANI
    SWALI KWA MWINYITANDI
    WAPI KWA KUGHANI

    NIMEISHI NYUMBANI
    PIA UGHAIBUNI
    NYUMBANI NI NYUMBANI
    LAKINI HURU SI NYUMBANI

    NIKIKUMBUKA KITIMOTO
    KACHUMBARI KWA MATANGO
    WACHILIA MBALI MAWAZO
    KWA MAMA NA MTOTO

    UGHAIBUNI SIO KWANGU
    NYUMBANI NDIO KWANGU
    JAPOKUWA MAISHA NI MACHUNGU
    MIE SIWEZI ELEZA SABABU

    UJANGILI UMEONGEZEKA
    UMASIKINI UMEKUWA
    RIZIKI KUCHAKUA
    KUKOSA NI MAUA

    NIMEBUNI BIASHARA
    WAKAJA THANASHARA
    WAKASEMA BIDHAA MARIDHAWA
    WAKAISHIA MACHO KUNAWA

    WAKAJA WALE WA VIBANDA
    KUNAWA KUTAKA KULA
    WAKAISHIA KUNAWA
    SIJUI NINI MARIDHAWA

    NIKAJIKALIA ZANGU KIBARAZANI
    NIKAWAZA NA KUFIKIRI
    MWANANCHI NALIPA KODI
    WAKATI BIASHARA HAILIPI

    NIKAJARIBU BONGO FLAVA
    TUKATENGENEZA PIA NA MAGITAA
    NAKALA KOPI KADHAA
    WADOSI WAKACHIKICHIA!
    ZAMANI NILICHEZA MPIRA
    KABLA YA SANDE MANARA
    ILIKUWA NI USHUJAA
    KUBURUDISHA SI KUTAFUTA!

    WAMESEMA NIKALIME
    TAIFA NILILISHE
    UCHUMI NIUJENGE
    MAISHA BORA NIPANIE

    WAKATOKA WALE MJINI
    WAMEKUJA NA GARI YA OFISI
    MAHINDI WAKAYATAMANI
    BEI YAKE HAWAKUTAMANI

    WAKALILIA NISHUSHE BEI
    ILI WAIMUDU BEI
    NIKAWAPA KWA ILE BEI
    WAKAFURAHI KAMA SI KUNIKEBEHI

    SASA MTOTO AMERUDI
    SHULE ILE YA JIONI
    WALIMU HAWAMUONI
    AMESHINDWA KULIPA MONI

    SASA MIMI NIFANYAJE
    KULIMA NIMELIMA
    KIPAJI NIMETUMIA
    BIASHARA NIMEFANYA
    MALIPO SIJAYAPATA

    NYIE HUKO MJINI
    AJIRA ZA SEREKALI
    DOLA IMEPANDA CHATI
    MSHAHARA HAUPANDI
    MATATIZO NIBEBE MIMI?

    KAMA MBOLEA NINANUNUA
    PEMBEJEO PIA NANUNUA
    USAFIRI NATUMIA
    MBONA MAHITAJI KAMA YENU?

    AKAJA BWANA KIKWETE
    LABDA ATANIONA MIMI KIWETE
    MATATIZO ANIFUMBULIE
    KURA NIMEMPA YEYE
    ALISEMA UPINZANI UTAONGEZA KASHESHE



    WANANAFASIHI MUNISAIDIE
    NINI CHANZO CHA KASHESHE
    UPINZANI HULETA KASHESHE
    AU KASHESHE HUSEMA KAPINGANE ?

    ACHA KASHESHE NINAISHI KWA KASHISHI
    NASTAHILI KUBWA BAKSHISHI
    LAKINI SWALI NATABARUKI
    KASHESHE LANGU HADI LINI ?

    KIKWETE NILIMUUNGA MKONO
    ALINIJIBU NILIPOMPUNGIA MKONO
    NAAMINI ATANIUNGA MKONO
    HATA KAMA KUNA CHOKOCHOKO ?

    ReplyDelete