Ads (728x90)

Bado nipo ningalipo,nijapo ndaja kwa tapo,
Naandaa yaliyopo,yaje barizi tulipo,
Tutambe yaso matapo, tuyaunde yaliyopo,
Fasihi njema zi papo, umma blogu usihofu.

Post a Comment

  1. Nasi twakutazamia
    Uje fikira jazia
    Lakini ukitulia
    Viboko takuchapia

    Tena wazi tamkia
    Nyumba ndogo kimbilia
    Lini utajarudia
    Nyumba kubwa kutunzia?

    Tumechoka kusikia
    Wanao kutwa lilia
    Chakula wakikosea
    Babayo mbali lowea!

    ReplyDelete
  2. Kweli uloyasemea, Makene nimesikia,
    Fikira nitajazia,Blogu tafurahia,
    Nyumba ndogo sina nia, Blog taimarishia,
    Mswada naandalia, Fasihi ilo tulia,
    Wana waje furahia, kaburi nikiingia,
    Wasome na kujivunia, ya blogu kutokea.

    ReplyDelete
  3. Nangoja huo muswada, ewe mwandishi mvivu
    Vipi njaa ulie shinda,tupa kunako uvungu
    Nona washindwa kesha, kalamu yawa machungu
    Mkwinda ninakwachia, Riwayani kimbilia.

    ReplyDelete
  4. Kumradhi, maoni yangu hayakujipanga nilivyotaka:
    nangoja huo muswada, ewe mwandishi mvivu
    vipi ulie njaa shinda, kipaji tupa kunako uvungu?
    Mbona washindwa kesha,kalamu geuza machungu
    Mkwinda ninakwachia, Riwayani kimbilia.

    ReplyDelete
  5. Kumradhi, maoni yangu hayakujipanga nilivyotaka:
    nangoja huo muswada, ewe mwandishi mvivu
    vipi ulie njaa shinda, kipaji tupa kunako uvungu?
    Mbona washindwa kesha,kalamu geuza machungu
    Mkwinda ninakwachia, Riwayani kimbilia.

    ReplyDelete
  6. Mkwinda,
    acha uvivu we malenga!

    Nafuatilia mapambano haya ya mistari hii ya kishairi.

    ReplyDelete
  7. Nijapo nena kivivivu,wanenao warizevu,
    Nitambe wacheke mbavu, wana watezee ndevu,
    Kamwe si vivu na tambo tambo zangu endelevu, watakari wavivu na wajao na zao nguvu.
    Makene, Ndesanjo wajuvu wa tambo zino angavu.
    Natamati kutotamba nasubiri tambo angavu.

    ReplyDelete
  8. Makene Ndesanjo, nahitaji Changamoto kwa mswada nilkopandisha katika bLogu vipi mbona kimya mmenywea mlidhani natania nilipowaambia kuwa naandaa mswada? haya kazi kwenu tugangamale tutoa kitabu kitokanacho na wanaBlogu

    ReplyDelete