Ads (728x90)

nyembo 6:21 PM
Uzongwapo na mizongo,usitarazie zongo,
Ikurubie mipango,uandaapo malengo,
Uuepuke uongo,ulijenge bora jengo,
Uzongwapo zongamana,ushikwapo shikamana.

Post a Comment

  1. uzongwapo zongamana,Mkwinda umelinena,
    zongo hilo gumu sana,kama hadithi ya jana?
    Kipi kilokuzongana,maneno kuyabetana?
    ama zongo tentana,karibu ya mautana?

    ReplyDelete
  2. Zongo hili zing zong, la mambo kutowiana,
    Utaraziapo zongo,wana tumbo vimbiana,

    Zongo lizongwapo zongo, matatizo tatizana,
    Hutamania mizengo,maisha kutafutana,

    Tukawa ja Bwana Mazengo, kutwa jua mvua ombea wana,

    Si mema yalo mazongo, kwa mola tuombeana.

    ReplyDelete
  3. Du! kijana kwa mashairi hayo, ninaimani Nyembo mwenyewe kachemsha kwani mi namfahamu sana mbovu mno kwa kiswahili!

    ReplyDelete