Nadhani tukio la hivi karibuni la Mwana wa 'Kukaya'Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 'JK' kulizungumzia suala la filamu ya Darwins Nightmare ya Bw. Hubert Sauper limechukua na kuhamisha fikra za wadanganyika.
Mimi nadhani watunzi wa riwaya na tamthiliya tutakuwa katika wakati mgumu kwa kuzuiwa kutoa kazi za kisanii na kifasihi kwa kuhofia dhana ya kuvuka mipaka ya fikra kwa matukio halisi yaliyopo.
Inakuwa ngumu kuchangia suala hili kabla ya kuiona filamu hiyo lakini kikubwa ni kwamba utunzi wa tamthiliya ni ubunifu wa kisanii uliochagizwa na fikra binafsi za mtunzi kwa mnasaba wa matukio halisi yanayojiri katika jamii.
Hebu wanablogi waliobahatika kuiona filamu hiyo watudadavulie yaliyomo ndani ya filamu hiyo ili tuanze kuchanganua kilichopo tujue pumba zipi na mchele upi, naamini,akina Sultani Tamba na wengine waliomo ndani ya Blogi wataungana nami kulichangia hili.
Wakatabahu
Mjadala huu, hotuba ile na yanayoendelea kwa wakati huu, ni ishara ya wazi kuwa kuna tatizo mahali, ama kwa uongozi, mitizamo, mapokeo ya changamoto au mahali fulani, lakini kwa ujumla yote yanayojiri ni ishara za mapungfu mahali fulani.
ReplyDelete