Nilitaka kusema, nikashikwa na kigugumizi lakini hata hivyo nilijikuta nasema ingawa nikashikwa mdomo na sheria ya kutoingilia mahakama, bali nadhani hakuna mahakama inayofanya kazi zake kisheria kufuata maoni na vishawishi vya watu wa mitaani.
Naamini mahakama zote zinafanya kazi kwa mujibu wa sheria na zinatoa haki kulingana na makosa husika bila kufuata ushawishi wa chombo chochote au maoni ya watu wa mitaani.
Hapa nina nia ya kulisema jambo hili ambalo magazeti ya Tanzania yamelivalia njuga kwa kipindi hiki ambacho serikali imepania kupigania haki za wanyonge kwa nguvu mpya kasi mpya na ari mpya.
Maskini Bro.Dito mtoto wa Ramadhani Mwinshehe wa Mzuzuri Born Town kitendo kilichomfika kinataka kuingia katika mkumbo wa kisiasa sijui kwa kuwa naye ni kijana kada aliyelelewa na siasa na kufika hapo alipo inasikitisha bali inaumiza familia ya Bin Mbonde ambaye amepoteza uhai wake bila hatia.
Hakustahili kuuawa bali sheria ya usalama barabarani ingefuatwa lakini si kama vile ilivyotokea kwa kiongozi mkuu kama Bro.Dito kuchomoa bastola na kumlenga shabaha dereva wa daladala kichwani.
Sijui ilikuwaje na wala sitaki kufikiria jinsi ilivyokuwa patashika kwaabiria waliokuwa wakiendeshwa na marehemu Mbonde wakati huo, mie nadhani walihisi basi limevamiwa na majambazi ambao hatimaye huenda wangeamrishwa kulala chini na kuvuliwa nguo zao.
Mie nadhani kilichofanyika hakikudiriki hasira kiasi hicho, au basi mkuu huyo angepiga risasi magurudumu ya gari lisiende mbele na hatimaye dereva angeshuka chini, bali kilichofanyika kwa kitendo cha kulipita gari kisha kulizuia lisiende na Mzee Dito kushuka kunako gari na kutoa cha moto.
Inatisha na nachelea kuendelea kusema kwa kile nilichokisema awali tumefungwa mdomo na sheria tuiache mahakama itende haki!!!!!!!!!
Ilianza kwa mkuu wa wilaya kumpiga mwenyekiti vibao, ikaja kwa RPC kuwatandika viboko wananchi imekuja kwa RC kuchomoa bastola na kumuua dereva wa daladala, itakuwaja kwa Waziri sijui atafanya nini..... na nanihii atafanya nini na nani hii atafanya nini mwishowe watu wataamua kujitoa muhanga ni hatari haki isipotendeka huu ni mtazamo wangu sidhani kama sheria inaweza kufuata mtazamo wa mtu na kuufanyia kazi.
Nakubaliana nawe kuwa nguvu na kasi mpya lazima ziendane na fikra mpya. Lakini hata hizo nguvu na kasi mpya zinazotajwa kila dakika ziko wapi? Kuna mtu mwenye mifano ya nguvu na kasi mpya ya serikali yetu?
ReplyDelete