Vijana hawa wadogo wenye umri wa kuwepo shuleni wakiwa katikaa harakati za kuosha magari barabarani na kupewa ujira kidogo kutoka kwa mwenye gari akipenda kufanya hivyo.Wanachofanya watoto hawa maarufu katika mtaa wa Uhindini jijini Mbeya.
Kila wanapoliona gari limeegeshwa wao hukimbilia wakiwa na ndoo za maji na vitambaa na kuanza kulisafisha bila mapatano na mwenye gari, akitokea mwenye gari humuonesha gari lake jinsi lilivyong'ara na kumuomba atoe chochote kutokana na kazi waliyoifanya, wengine hutoa elfu moja wengine mia tano, wengine hutoa mia mbili na wengine hawatoi chochote.
Wale wanaotoa chochote vijana hao hushukuru na kwa yule asiyetoa chochote hatimaye huambulia matusi kutoka kwa vijana hao jambo ambalo limekuwa ni kero kwa wakazi wa jijini Mbeya, kwani kwanza kazi hiyo huifanya bila makubaliano.Kazi kwenu askari wa jiji la Mbeya.
Post a Comment
Post a Comment