Ads (728x90)

Kama mjali, wa taa,maisha yalivyo,
Ni muhali, kukaa, vivyo ulivyo,
Kwa kila uwakavyo huisha vivyo.

Maisha kama tambara, bovu liishavyo,
Hayahitaji papara, na nguvu isivyo,
Kadiri uishivyo, ndivyo yaishavyo.

Uishi vyema na watu kadri ilivyo,
Uwe mwema, kwa utu,daima ndivyo,
Ya dunia ndivyo, maisha yalivyo.

Uwe na njema, tabia, uendavyo,
Ichunge huruma, zingatia, uwezavyo,
Ya akhera mandalizi, wako ujuvyo.

Ibada kwako, ni hima si ya upuuzo,
Kuikosa mwiko, lazima marejelezo,
Zingatia makatazo, ya Karima.

Kwa magego, ukamate,iwe zingatio,
Siupe mgongo, ujute na muishio,
Kwangu malizio kwa waadhi huno.

Wakatabahu.

Post a Comment

Post a Comment