Ads (728x90)

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA IKIONEKANA KABLA YA KUBOMOLEWA

JANA katika FB niliweka picha hii ya kigogo mmoja hapa nchini ambaye ameamua kujenga nyumba hii ya biashara katika eneo ambalo ni kwa ajili ya matumizi mengine.
Baada ya kumfuata Meneja wa TANROAD mkoa wa Mbeya Bw.Lucian Kilewo na Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya Bw.Juma Rashid nikapata maelezo yanayokinzana ambapo Mkurugenzi alisema kuwa nyumba imejengwa katika nyumba iliyokuwepo awali,Meneja wa Tanroad anasema eneo lile halikutakiwa kujengwa nyumba mpya kwa kuwa ni hifadhi ya barabara.
Hata hivyo Bw. Kilewo alisema kuwa wakati ujenzi unaanza TANROAD ilizuia ujenzi huo lakini hata hivyo ujenzi huo uliendelea hatimaye leo nyuma imebomolewa, kama inavyoonekana katika picha.



BOMOA BOMOA INASHIKA KASI

Post a Comment

Post a Comment