BAADHI YA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU WAKIOMBA DUA MARA BAADA YA KUSWALI SWALA YA IDD EL FITRI KATIKA MAENEO YA KWIANJA NGOMA SOKOMATOLA JIJINI MBEYA IKIWA NI KUKAMILIKA KWA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI, HATA HIVYO WAUMINI WENGINE WA DINI YA KIISLAMU WANAENDELEA NA MFUNGO HADI HAPO KESHO.
TAARIFA ZA KUANDAMA KWA MWEZI MFUNGO MOSI AMBAZO NI KUKAMILIKA KWA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI ZIMEENDELEA KUMIMINIKA KATIKA BLOGU HII AMBAPO MKAZI WA WILAYANI MASASI MKOANI MTWARA ALIYEJITAMBULISHA KWA JINA LA NURDIN ABUBAKAR ALISEMA KUWA WALIPATA TAARIFA ZA KUONEKANA KWA MWEZI MARA BAADA YA KUSWALI SWALA YA MAGHARIBI AMBAPO YEYE PAMOJA NA KUNDI LA WATU WALIUSHUHUDIA MWEZI KWA MACHO YAO KATIKA MAENEO YA MJINI, KITONGOJI CHA WAPIWAPI MISUFINI,MKUTI MAENEO YA KWA ROBEN, JIRANI NA STEND YA MABASI.
MAHOJIANO BAINA MWANDISHI WA BLOG HII NA SHUHUDA WA MWEZI YALIKUWA KAMA IFUATAVYO:
MWANDISHI: HALOO ASSALAAM ALAYKUM,NA KWA FAIDA YA WASOMAJI NITAJIE JINA LAKO!!
SHUHUDA: WAALAYKUM SALAAM HABARI ZA HUKO,MIE NAITWA NURDIN ABUBAKAR MKAZI WA MASASI SHUGHULI ZANGU NAFANYIA STENDI YA MABASI HAPA MASASI!!!IDD MUBARAK SISI NDIO TUNATOKA KUSWALI IDD HAPA VIPI HUKO KWENU MMESHASWALI.
MWANDISHI: WAALAYKUM SALAAM NASI HUKU TULIKO TUMESHASWALI, HUKU NI KWEMA TUNAMSHUKURU MUNGU...EHEE NIPE TAARIFA ZA KUONEKANA KWA MWEZI
SHUHUDA: MWEZI UMEONEKANA KATIKA VITONGOJI VINGI IKIWEMO KITONGOJI CHA WAPI WAPI,MISUFINI, MKUTI KARIBU NA KWA ROBEN, MAMA MMOJA ALIENDA KUTOA TAARIFA KWA SHEKHE WA MKOA WA MTWARA AMBAYE MAKAZI YAKE YAPO HAPA MASASI NA KUNDI KUBWA LA WATU LILIENDA PAMOJA NA HUYO MAMA ILI KUTOA TAARIFA WAKIWA NDANI YA GARI AINA YA TOYOTA JILUX MALI YA BWANA MMOJA ANAITWA BAKIRI.
MWANDISHI/>: EHEE NINI KILIENDELEA BAADA YA HAPO, SHEKHE WA MKOA ANAITWA NANI?
SHUHUDA: SHEKHE WA MKOA ANAITWA JINA LA KWANZA SAID JINA LA PILI NI...NI... MKUMBA NAAM ANAITWA SHEKHE SAID MKUMBA YEYE NDIYE SHEKHE WA MKOA BAKWATA MAKAZI YAKE YAPO HAPA MASASI.
MWANDISHI: BAADA YA KUFIKA KWA SHEKHE NINI KILIFUATA!!!
SHUHUDA: BAADA YA KUFIKA KWA SHEKHE KUNDI LA WATU KAMA KUMI WAKIWEMO MAMA MMOJA ANAITWA HAMIDA ABDALLAH AMBAYE ALIUONA MWEZI KWA MACHO YAKE MAENEO YA MISUFINI, PAMOJA NA MUMEWE,PIAA ALIKUWEPO BWANA ABDUL NADIRIKA AMBAYE ALIUONA MWEZI KARIBU NA SHULE YA MSINGI KAMBARAGE WALIFIKA NYUMBANI KWA SHEKHE WAKAMKUTA NA KUTAKA KUAPISHWA ILI KUTHIBITISHA KUWA WAMEUONA MWEZI.
MWANDISHI: NAAM BAADA YA HAPO ILIKUWAJE?
SHUHUDA:WALIMUELEZA SHEKHE,NAYE AKASEMA KUWA HANA MAMLAKA YA KUUTANGAZA MWEZI BALI ATAMPIGIA MUFTI WA TANZANIA SHEKHE ISSA SHAABAN SIMBA ILI ATANGAZIE UMMA WA WAISLAMU KUWA MWEZI UMEONEKANA.
MWANDISHI: HUYO SHEKHE ALIMPIGIA SIMU MUFTI?
SHUHUDA: KWA KWELI HATUFAHAMU KAMA ALIMPIGIA SIMU MUFTI AMA LA!! HIYO IMEBAKI KUWA NI DHIMA YAKE MBELE YA MWENYEZI MUNGU LAKINI SISI TULIFANYA JITIHADA ZA KUTOA TAARIFA ZA KUONEKANA KWA MWEZI AMBAO TULIUONA KWA MACHO YETU NA HIVI TUMETOKA KUSWALI KATIKA VIWANJA VYA IMAMU MALIKI HAPA MASASI NA WENGINE WAMESWALI KATIKA VIWANJA VINGINE HUKU SISI LEO TUNASHEREHEKEA IDD EL FITRI.
MWANDISHI: UNAWEZA KUNIFANYIA JITIHADA NIKAPATA NAMBA ZA SIMU ZA SHEKHE WA MKOA TAFADHALI!!
SHUHUDA: INAWEZEKANA LAKINI NAOMBA UNIPE MUDA HADI HAPO BAADAYE NIITAFUTE NIPIGIE BAADAYE INSHAALLAH NITAKUWA NIMEIPATA KWANI HAISHI MBALI.
HIZO NDIZO TAARIFA ZA KUONEKANA KWA MWEZI HUKO MASASI KAMA ZILIVYOONEKANA JANA.
TUTAENDELEA KUKULETEA MAHOJIANO YA SHEKHE WA MKOA WA MTWARA MARA BAADA YA KUPATIKANA HAPO BAADAYE!!!
Post a Comment
Post a Comment