KWA MUJIBU WA TAARIFA ZA WATU KUTOKA WILAYA YA MASASI MKOANI MTWARA NI KWAMBA MWEZI WA MFUNGO MOSI UMEANDAMA IKIWA NI KUKAMILIKA KWA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN, HATA HIVYO TAARIFA HIZO ZIMEPINGWA NA VIONGOZI WA BAKWATA KUPITIA KWA SHEKHE WA MKOA WA DAR ES SALAAM ALHAD MUSSA KUPITIA RUNINGA YA TBC AKIDAI KUWA TAARIFA HIZO ZIMEPANDIKIZWA NA MEDIA YA KIISLAMU (RADIO IMAAN FM) YENYE MSIMAMO WA KUFUNGA KWA MWEZI UNAOANDAMA NA NCHI ZINGINE TOFAUTI NA NCHI ZILIZOKARIBU NA NCHI YETU.BLOG HII IMEJITAHIDI KUWASILIANA NA WATU WA MASASI TAKRIBANI WATATU AMBAO WOTE KWA PAMOJA WAMETHIBITISHA KUONEKANA KWA MWEZI HUO. TAARIFA KWA UKAMILIFU JUU YA MAHOJIANO NA WATU HAO WA MASASI ZITAWEKWA HAPA KESHO.
AIDHA KULINGANA NA TAARIFA KUPITIA KITUO CHA RADIO YA KIISLAMU CHA RADIO IMAAN FM NI KWAMBA MWEZI UMEONEKANA KATIKA MJI WA MECCA SAUDI ARABIA AMBAKO KALENDA NA SAA YAKE HAITOFAUTIANI NA YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI NA PIA UMEONEKANA NCHINI MALASIA.
Post a Comment
Post a Comment