36 WASHAMBULIWA NA KUFA NCHINI BURUNDI
Watu wasiofahamika wamefanya shambulio na kuwaua watu 36 katika Klabu moja iliyopo eneo la Gatumba mpakani mwa DRC na Burundi usiku wa kuamkia leo.
RAIS WA BURUNDI BW.PIERE NKURUNZINZA(PICHANI KULIA)
Watu hao wasiofahamika ambao walivalia mavazi ya kijeshi walivamia Klabu hiyo maarufu kwa jina la Kilabu Cha Marafiki na kuua watu hao kwa risasi ambapo taarifa zinadai kuwa mauaji hayo inawezekana kuhusishwa na kundi la waasi wa nchini humo.
MMOJA WA MAJERUHI ALIYENUSURIKA AKIPATIWA MATIBABU NCHINI BURUNDI
RAMANI YA NCHI YA BURUNDI
Kufuatia mauaji hayo Rais Piere Nkurunzinza ambaye alitakiwa kwenda nchini Marekeni kwa ziara ya kikazi aliahirisha ziara hiyo na kutangaza siku tatu za maombolezo.
Source/ BBC
Post a Comment
Post a Comment