Watu watatu wakiwemo wabunge wawili wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wamepandishwa kizimbani katika mahakama ya mkoa Tabora kwa kosa la kumdhalilisha Mkuu wa wilaya ya Igunga Bi. Fatma Kimario.Washitakiwa hao ambao ni Mbunge wa Maswa Mashariki Bw.Sylvester Kasulumbai na Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Morogoro Bi.Suzan Kiwanga pamoja na Bw. Annuary Kashaga walifkishwa katika mahakama hiyo na kusomewa mashtaka manne ya shambulio,wizi,kutoa lugha ya matusi na kumuweka chini ya ulinzi kinyume cha sheria.
Walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama ya Tabora Bw.Thomas Simba na kusomewa mashtaka ambayo wote kwa pamoja walikana mashtaka yao.Washitakiwa hao wanatetewa na Mbunge wa Singida Bw.Tundu Lissu wako nje kwa dhamana ya shilingi milioni tano kila mmoja.
Post a Comment
Post a Comment