Ads (728x90)

INSPEKTA JENERALI WA POLISI BW.SAID MWEMA
Kwa muda mrefu mkoa wa Mbeya umekuwa ukizizima kwa matukio ya uhalifu ambapo wakati ule kamanda wa polisi mkoa alikuwa Bw. Said Mwema ambaye kwa sasa ni IGP yaliibuka matukio ya ajabu na kuibua hisia za imani za ushirikina ambapo watu walichunwa ngozi, kunyofolewa sehemu za siri na matiti hali hiyo ilidhibitiwa na kuwa shwari.
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR BW. SULEIMAN KOVA
Aidha katika kipindi cha Kamanda wa Polisi Bw. Suleiman Kova ambaye kwa sasa ni Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es salaam, yaliibuka tena matukio ya aina hii ambapo kufuatia dhana ya ulinzi shirikishi na polisi jamii iliyokuwa ikifanywa na kamanda Kova katika ngazi ya Kata hatimaye matukio hayo yalianza kudhibitiwa na kupungua.
KAMANDA WA POLISI MKOA DODOMA BW. ZELLOTHE STEPHEN
Katika kipindi cha Kamanda wa Polisi Bw.Zellothe Stephen yaliibuka tena matukio hayo sanjari na ujambazi wa kutumia silaha lakini hata hivyo kwa dhana ile ile matukio hayo yalipunguzwa na hali ilirejea tena kuwa shwari kwa wakazi wa Jiji la Mbeya na mkoa kwa ujumla.
KAMANDA WA POLISI MKOA MBEYA ADVOCATE NYOMBI
Matukio hayo baada ya kusimama kwa muda mrefu yamerejea tena kwa kasi katika kipindi hiki ambacho kamanda wa polisi Bw. Advocate Nyombi akiwa na mikakati ya kupunguza uhalifu kwa dhana ile ile ya ulinzi shirikishi na polisi jamii, huku kukiibuka wimbi kubwa la Vijana waliojiajiri katika sekta binafsi maeneo kadhaa ya Jiji la Mbeya wakifukuzwa katika maeneo hayo na Halmashauri ya Jiji na kuamuriwa kuondoka.
UOSHAJI MAGARI UNAVYOPIGWA VITA MAENEO MBALIMBALI NCHINI

Kasi ya vijana hao kuondolewa katika Vijiwe vya kuoshea magari kama vile Sinde, Mafiat na maeneo mengine ya Uyole limeelezwa kuwa ni tatizo kwa kuwa vijana hao walikuwa wakijipatia kipato na kuendesha maisha yao na familia zao kwa kuosha magari hali ambayo kwa sasa imetoweka na kuwafanya vijana hao kuingia katika uzururaji.
MKURUGENZI WA JIJI LA MBEYA BW. JUMA IDD RASHID

Ikumbukwe kuwa maeneo ya kuoshea magari na vijiwe vya Machinga ni sehemu ya vyanzo vya mapato vya vijana hao lakini kutokana na mpango wa Jiji kuwaondoa vijana hao vyanzo hivyo vya mapato vimetoweka na kujengeka dhana kuwa huenda vijana hao waliokuwa wakijipatia kipato kwa jasho lao kupitia ubunifu wao wa ajira isiyo rasmi ya uoshaji wa magari,kukosa ajira hiyo ndio wamekuwa chanzo cha uhalifu.
MOJA YA ATHARI ZA UPIGAJI WA NONDO KAMA INAVYOWAKUMBA VIJANA NAMNA HII
Ni vyema ukawekwa mkakati wa kuwaboreshea maeneo yao vijana hawa badala ya kuwatimua kama ilivyofanyika hv sasa ambapo tumekuwa tukisikia kila siku kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja watu kadhaa wameuawa kwa kupigwa nondo na wengine chungu nzima wakiwa wamelazwa hospitali ya rufaa wakiwa hoi kwa majeraha ya kupigwa nondo.

Post a Comment

Post a Comment