Ads (728x90)

Waziri Emmanuel Nchimbi aombwe radhi kwa lipi katika sakata la uchaguzi wa meya Songea?

Baada ya Jumamosi ya 24.9.2011 kuripoti kuhusu Emmanuel Nchimbi kukimbia na sanduku la kura, baada ya mzozo wa kuchakachua kura za umeya, leo amawaita waandishi wa habari na kukanusha kuwa yeye hakufanya kitu kama hicho. Na magazeti ya Tanzania Daima, Mwananchi na Majira yaliyoripoti habari hiyo yameatakiwa kumwomba radhi katika kurasa za mbele za matoleo ya jumatatu kesho 26.9.2011.

Ukweli ni kwamba kama ilivyoripitiwa na magazeti hayo na pia sisi tulioshuhudia tukio hilo Ijumaa hatuoni sababu ya magazeti hayo kufanya hivyo kwani ni dhahiri Nchimbi alifanya kitu hicho. Labda tuseme Bwana Nchimbi atumie tu cheo chake cha Uwaziri wa habari kutaka kuyalazimisha magazeti hayo kufanya hivyo. Vinginevyo ni habari zilizo na usahihi kabisa wala waandishi hawakutunga. Labda wahariri wa magazeti hayo waamue kuufyata kwa Nchimbi.

Ndugu zangu vitendo vya kimafya kwenye chaguzi hapa songea Nchimbi ni bingwa wa kufanya hivyo. Uongozi anataka yeye ndio aupange. Na anawaweka watu wasio na kisomo ili awaburuze. Mfano, Ndugu G Ndimbo ndiye aliyesoma na mwenye uelewa sana katika madiwani wote ambaye kipindi cha 2005 hadi 2010 ndiye aliyekuwa meya. Sasa huyu kutokana na usomi wake hawakuwa anaburuzwa. Kuona hivyo Nchimbi akamfanyia zengwe asipite tena. Akampandikiza Darasa la Saba Marehemu Manya. Hata huyu mama Mariamu Dizumba naye ni boya hana elimu. Hivyo anaburuzwa tu na Nchimbi.
Kwa maoni yangu, magazeti hayo hayana sababu ya kumwomba radhi, habari hiyo ilikuwa sahihi kabisa. Labda tu wamwogope.

Na hapa nimwombe ndugu Gerson Msigwa kuacha ushabiki wake kwani alitakiwa kuripoti taarifa ile. Sina hakika kama aliripoti kwan Songea hatukuwa na umeme maeneo mengi ya mji huu kwa siku tatu mfululizo.SHivyo sijui kama alitoa hewani habari hiyo.Hapo naomba nifahamishwe. (STORI KWA HISANI YA JAMII FORUMS)

Post a Comment

Post a Comment