KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA BW.ADVOCATE NYOMBI AKITOA HESHIMA ZA MWISHO LEO ASUBUHI MBELE YA JENEZA LENYE MWILI WA ASKARI POLISI MESHACK URASSA ALIYEUAWA KWA KUPIGWA NONDO JUZI USIKU
TAARIFA za kukithiri kwa upigaji wa nondo katika mkoa wa Mbeya kumeendelea kuutia hofu mkoa huo ahali ambayo inasababisha wananchi wasiztishe matembezi ya usiku na kuamua kuingia majumbani mwao mapema.
Mwandishi wa Blog hii ameshuhudia wakazi wa Jiji la Mbeya na Wilaya ya Mbozi wakirudi majumbani kuanzia saa 12 jioni wakihofia kukumbana na kadhia ya kupigwa nondo ambapo usiku wa kuamkia jana askari polisi Meshack Urasa ameuawa kwa kupigwa na nondo na kundi la watu wasiofahamika.
Aidha makundi ya majeruhi wamefurika katika hospitali ya Rufaa Mbeya na ile ya wilaya ya Mbozi iliyopo mjini Vwawa kutokana na watu kuendelea kupigwa nondo na watu wasiofahamika huku jitihada za ufumbuzi wa tatizo hilo zikiwa bado kitendawili.
RPC MKOA WA MBEYA ADVOCATE NYOMBI
Post a Comment
Post a Comment