Ads (728x90)

RAIS WA AWAMU YA TATU BW.BENJAMIN MKAPA AKIMNADI DKT DALALY KAFUMU MGOMBEA WA CCM ALIYESHINDA UCHAGUZI MDOGO WA JIMBO LA IGUNGA

HATIMAYE baada ya mvutano wa muda mrefu na kampeni ya siku 21 kuziba pengo la Ubunge jimbo Igunga lililoachwa wazi na Bw.Rostam Aziz,leo saa 9:00 Alasiri msimamizi msaidizi wa uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga Bw.Protace Magayane amemtangaza mgombea Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt.Dalaly Kafumu kuwa mbunge wa jimbo la Igunga baada ya kupata kura 26,484 kati ya kura 53,672 zilizopigwa kati ya wapiga kura 171,019.

MSIMAMIZI WA UCHAGUZI PROTACE MAGAYANE

Mgombea wa CHADEMA Mwalimu Joseph Kashindye alipata kura 23,260.
MGOMBEA WA UCHAGUZI KWA TIKETI YA CHADEMA BW.JOSEPH KASHINDYE

Mgombea wa CUF Bw.Leopold Mahona aliyeambulia kura 2104 huku vyama vingine vikiambulia kura chache AFP kura 235, CHAUSTA kura 182,DP kura 76, SAU kura 83 na chama cha UPDP kura 63.

MWENYEKITI WA CUF PROF.IBRAHIMU LIPUMBA AKITETA JAMBO NA MGOMBEA UCHAGUZI KWA TIKETI YA CHAMA HICHO BW.LEOPOLD MAHONA

Post a Comment

Post a Comment