HII NI AINA YA NYUMBA WANAZOISHI ASILIMIA KUBWA YA WATU WAISHIO VIJIJINI AMBAO HURIDHIKA NA MAISHA HAYA, NA HAYA NDIYO AINA YA MAISHA YAO NA HUKUBALI KUWA NDIO MAISHA BORA.
SHIDA INAPOKITHIRI WAZEE KAMA HUYU HULAZIMIKA KUFANYA VIBARUA KWA WENYE UWEZO WA KUMILIKI MASHAMBA ILI ANGALAU WAWEZE KUJIPATIA FEDHA YA SABUNI NA HATA KARO YA SHULE KWA WATOTO
MARA NYINGINE HATA UPATIKANAJI WA CHAKULA UNAKUWA SHIDA KUTOKANA NA WANANCHI WENGI WA VIJIJINI KUUZA AKIBA YA CHAKULA CHOTE NA HIVYO KULAZIMIKA KUZOA AKIBA INAYODONDOKA CHINI NA KUPEPETA KAMA ANAVYOONEKANA BIBI HUYU HUKO VIJIJINI.
HUDUMA YA MAJI NI YA SHIDA AMBAYO HATA INAPOPATIKANA MAJI YAKE SI SALAMA KWA KUNYWA BALI WANALAZIMIKA KUNYWA, WENYE KUELEWA AFYA HUCHEMSHA NA WALE WASIOELEWA HUAMUA KUNYWA HIVYO HIVYO BORA LIENDE
ILI KUPATA HUDUMA ZA HOSPITALI UNALAZIMIKA KUTUMIA BAISKELI UKIWA UMEWABEBA WATOTO WAWILI WANAOUMWA NA KUTEMBEA UMBALI WA ZAIDI YA KILOMITA 30.
MTOTO AISHIYE MJINI HAFANANI NA YULE AISHIYE KIJIJINI, MJINI ANAPATA FURSA MBALIMBALI ZA KIMAISHA IKIWA HATA KUFURAHI NA KUCHEZA FURSA AMBAYO MTOTO WA KIJIJINI HAIPATI.
KUELEKEA KIJIJINI SHARTI UPITE KATIKA DARAJA HILI AMBALO CHINI YAKE KUNA MTO WENYE MAJI YA KINA KIREFU CHENYE MAMBA WENYE NJAA KAMA UNA KIZUNGUZUNGU HUWEZI KUVUKA MTO HUO.
WACHACHE TUISHIO MIJINI TUNAPENDA KULIMA NA HATA KUFUGA ILI KUJIPATIA NG'OMBE WA MAZIWA KWA AJILI YA AFYA ZETU LAKINI FURSA HIZO ZINAKUWA ADIMU NA KUENDELEA KUBAKI KUISHI KAMA TULIVYO TUKISUBIRI KUOMBA URAIA KATIKA NCHI ZA WENZETU TUKIDHANI KUWA HUKO NDIKO KWENYE MAISHA KAMA YA PEPONI.
Post a Comment
Post a Comment