Ads (728x90)

MARA zote watu hupima uwezo wao wa mali na kujifananisha na wale wasio na mali, uwezo wa mmoja ndiyo sababu ya mwingine kunufaika na uwezo ulionao, si vyema kudhani kuwa uwezo ulionao ni ujanja wako, kwani Mungu ameumba dunia mduara kilichopo leo hapa kesho kitakuwa upande mwingine, na ili dunia iende kumekuwepo matabaka wa walio nacho na wale wasio nacho, iko siku wale wasio nacho watakuwa nacho na wale wenye nacho watakuwa hawana tena, hayo ndio maisha!! kupanda na kushuka.

Hekima ya Mungu kuwaruzku uwezo watu wengine na kuwanyima wengine ni kuweka uwiano wa kimaisha na hsa hiyo ndiyo dunia na maumbile yake, ingekuwaje kama kila mtu angemiliki nyumba nani angepanga? ingekuwaje kila mtu ana duka nani angenunua? ingekuwaje kila mtu anamiliki gari nani angetembea kwa miguu? na ingekuwaje kila mtu angekuwa kiongozi nani angeongozwa!!! huu ni mpango mahsusi uliowekwa na Mungu ili dunia iende na heshima iwepo mingoni mwa jamii!!! MAISHA NI KUPANDA NA KUSHUKA!!

Post a Comment

Post a Comment