Ads (728x90)

TUNAKUKUMBUKA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE NI MIAKA 12 TANGU UIAGE DUNIA UMEWAACHIA MAJONZI WATANZANIA WALIKULILIA SANA,HATA HIVYO UMEACHA PENGO KUBWA AMBALO LIMEZIBWA NA MAFISADI AMBAO WANA ITIKADI YAKO WANAIMBA KWA JINA LAKO, WANAKULA KWA JINA LAKO,WANATENDA KWA KUTUMIA JINA LAKO WANAJISIFU NA KUJIGAMBA WEWE NDIYE BABA YAO NA WANAAMINI KUWA WAKIFANYACHO KIMETOKANA NA MAFUNDISHO YAKO.

UMETIMIZA MIAKA 12 TANGU UONDOKE DUNIANI,YALIYOFANYWA KWA KIPINDI CHOTE CHA MIAKA 12 NI SAWA NA UHURU WA MANYANI,DHAMIRA ZAO HAZIFANANI NA MATENDO YAO WAKIFANYACHO KINASHABIHI DHANA YA UFISADI NA UFEDHULI ULIOPITUKA MIPAKA.

UMEONDOKA HUKU BADO UKIHITAJIWA NA WANANCHI NA HATA WANACHAMA WA CHAMA ULICHOKIASISI AMBACHO KWA SASA KIMEJAA WATAPIAJI KULA WANAOAMINI KUWA,WAO NDIO WAO NA WATAENDELEA KUDUMU MILELE KATIKA ENZI WALIZONAZO

Post a Comment

Post a Comment