Ads (728x90)

 Vilio na majonzi vilitawala katika maziko ya kijana Kevin Mwa;lingo mwendesha bodaboda ambaye aliuawa wakati wa vurugu za wamachinga na askari polisi baada ya kupigwa risasi ya moto wakati akitoka kujipatia cvhakula katika moja ya mgahawa jijini humo.
 Kevin (pichani juu) katolewa mhanga katika tukio ambalo halikumhusu kutokana na hali ya taharuki iliyoibuka juzi na jana wakati askari wa kutuliza ghasia walipoamua kutumia risasi za moto kuwadhibiti wananchi ambao walikuwa wakipinga kuondolewa katika maeneo yao ya biashara bila kutengewa maeneo mbadala.

 Umati wa watu waliohudhuria maziko hayo ambayo hata hivyo hakuna kiongozi yeyote wa juu wa serikali aliyekuja kutoa salamu za rambirambi zimeelezwa kuwa ni kiwango cha juu cha unyanyasaji unaoendelea dhidi ya raia wasio na hatia na lawama nyingi zinawaendea wapangaji wa mipango wa serikali ambao wanashindwa kuweka mkakati wa kuwapangia maeneo ya biashara wamachinga.
 Juzi na jana zilikuwa ni siku ambazo wananchi walishindwa kufanya shughuli zao kama kawaida baada ya vitongoji vya Jiji la Mbeya maeneo ya Uyole,Mwanjelwa na kwingineko kuibuka vurugu na mapambano baina ya wamachinga na askari polisi kutoka mikoa mitatu ya Nyanda za Juu kusini, hata hivyo hali hiyo imerejea kuwa shwari kama inavyoonekana pichani juu ambapo leo asubuhi shughuli zimeendelea kama kawaida.
(Baadhi ya wakazi wa Uyole wakishiriki maziko ya kijana Kevin aliyeuawa kwa kupigwa risasi katika mapambano kati ya askari polisi na wamachinga) (PICHA KWA HISANI YA DOTTO MWAIBALE)

Post a Comment

Post a Comment