|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. Yah;Kuibiwa kwa mwanahabari Thobias Mwanakatwe. UONGOZI wa Klabu ya Waandishi wa habari mkoa wa Mbeya(MBPC) unatoa tamko kali na kulaani tukio la wizi alilofanyiwa,Mwanahabari,Thobias Mwanakatwe usiku wa kuamkia siku ya Krismas 25/12/2011. Kwa taarifa hii na kwa kutambua ushirikiano mzuri uliopo kati ya wanahabari na jeshi la polisi ni matumaini yetu kuwa watuhumiwa wote waliohusika kwenye wizi huo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Kitendo cha Mwanakatwe kuibiwa mali zake zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 4.3 kimechangia kurudisha nyuma maendeleo yake kimaisha na kupunguza jitihada zake za kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa kwani miongoni mwa vifaa vilivyoibiwa ni vya kikazi kama,Laptop,kamera na tape recorder. Kwa taarifa hii tunajua fika kuwa mtaa wa Hiari ya Moyo kata ya Majengo anakoishi Mwanakatwe kuna uongozi thabiti na ni dhamira yetu kuona kuwa uongozi wa serikali ya mtaa na kata unawajua wahusika na miongoni mwao inawezekana ni wakazi wa maeneo hayo ambao watakuwa msaada mkubwa kwa jeshi la polisi. |
|
Tunalaani kitendo hicho sio tu kwa sababu kimemgusa mwanahabari,MBPC haifurahishwi kabisa na matukio ya aina yoyote ya uhalifu wanayofanyiwa wananchi na kuishauri jamii ipige vita matukio ya wizi,ujambazi,upigaji nondo na mauaji ya aina yoyote yanayosukumwa na imani za kishirikina. Ili wananchi waweze kuwa salama pia wanapaswa kutambua mchango mkubwa wa kihabari unaotolewa na waandishi wa habari katika mkoa wa Mbeya ni imani yetu kuwa vitendo viovu visiwe sehemu ya kuwatisha na kuwakatisha tamaa waandishi wa habari. Kwa kujua na kutambua hasara kubwa aliyoipata Mwanakatwe ni mategemeo yetu kuwa ndugu,marafiki na wadau wa habari watakuwa tayari kumsaidia kwa hali na mali,Mwanakatwe ili angalau aweze kurejea katika maisha yake ya kawaida yeye na familia yake. Kama tulivyosema,Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya likiongozwa na Kamanda mahiri,Advocate Nyombi haliwezi kushindwa kuwabaini wahusika ambani ni wazi kuwa mali zote zilizoibiwa bado zinazungushwa mitaani,pia tunategemea kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi. Taarifa hii imetolewa na, |
Mwenyekiti Mbeya Press klabu
Christopher Nyenyembe,
28/12/2012.
Post a Comment
Post a Comment