MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya Abel Motika aka Mr.Ebbo aliyefariki dunia mapema jana anatarajiwa kuzikwa jumatatu katika makaburi ya familia ya Boma la Motika Masai Camp yaliyopo huko mjini Arusha.
Mr;Ebbo amekuwa ni miongoni mwa wasanii mahiri waliopania pia kukuza vipaji vya wasanii wengine, alikuwa ni miongoni mwa wasanii wachache wenye vipaji adimu ambavyo vilipaswa kuigwa na wasanii wengine hapa nchini.
Atakumbukwa kwa kutokuwa na makundi ambapo muziki wake wenye lahaja na lafudhi ya lugha yake ya kimasai ulileta mvuto mkubwa kwa wapenzi wake wa ndani na nje ya nchi.
Post a Comment
Post a Comment