Ads (728x90)

 MWILI wa aliyekuwa mtangazaji wa Radio Tanzania Dar es salaam, RTD David Zimbihile Wakati umezikwa leo.
 Marehemu Wakati atakumbukwa kwa umahiri wake wa kutangaza vipindi mbalimbali, namkumbuka sana katika kipindi chake maarufu alichokuwa akikiendesha mwenyewe cha 'JIBU LAKO'
 Alikuwa mahiri katika mahojiano katika vipindi mbalimbali vya Redio na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakati huo wa chama kimoja.
 Marehemu wakati alikuwa karibu na viongozi wakuu wa serikali akiwemo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Atakumbukwa zaidi kwa ubunifu na uratibu makini wa vipindi ambavyo vilipendwa zaidi na hata wakati wa mfumuko wa vyombo huria vya habari vingi viliiga mtindo wa uendeshaji wa RTD.

Post a Comment

Post a Comment