Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Mbeya Bw. Ezekiel Mgeni akisimamia zoezi la kufungua namba za usajili za magari ambayo yanakiuka sheria za usalama baarabarani kama walivyokutwa na kamera yetu jioni hii katika barabara ya Lupa.
Utaratibu wa kufungua namba za usajili wa magari hayo umekuja siku chache baada ya kuwataka madereva watumiaji wa barabara hiyo kutumia kwa njia moja tu ya kuteremsha bila kupandisha ili kuzuia msongamano uliopo katika barabara hiyo maarufu ya UHINDINI.
Askari wa kikosi cjha Usalama barabarani mjini Mbeya akifungua namba za gari lenye usajili T304 AWF ambalo limeegeshwa kuelekea upande ambao hauruhusiwi kisheria katika barabara hiyo.
Trafiki akiwa kazini akitekeleza wajibu wake kwa madereva wakiukaji wa sheria za usalama barabarani
Askari wa Usalama barabari mjini Mbeya akifungua namba za usajili za gari T 317AGU ambalo lilikuwa liko katika uelekeo ambao hairuhusiwi kupita magari
This blog very interesting but you can also try these ..www.jigambeads.com and ..www.tanzaniakwetu.com for popularity and more advert to advertise. Thanks
ReplyDelete