Katibu Mkuu
wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Dkt.Wilbroad Slaa anatarajia
kutua Jijini Mbeya Januari 10 kwa ziara ya kuhamasisha chama mkoani humo.
Kwa mujibu
wa taarifa ya Katibu wa CHADEMA mkoani Mbeya Eddo Makatta anasema kuwa Dkt.
Slaa ataingia Jijini Mbeya na kufanya mikutano ya ndani kisha mikutano ya
hadhara katika maeneo mbalimbali ya wazi.
Makatta
alisema kuwa ziara hiyo ni moja ya mikakati ya chama hicho kukutana na wapiga
kura wake kwa nia ya ,kuwazindua juu ya mambo mbalimbali ya hujuma na ufisadi
dhidi ya wananchi unaofanywa viongozi waliopo madarakani.
Alisema kuwa ziara ya Dkt. Slaa inakuja wakati
kukiwa na mijadala na midahalo mbalimbali inayoendelea juu ya marekebisho ya
Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Post a Comment
Post a Comment