Kwa nini utumie Google Chrome?
Google Chrome ni kivinjari wavuti kinachoendesha kurasa na programu za wavuti kwa kasi ya umeme. Soma kuhusu ni kwa nini tuliunda kivinjari.Kasi: Huanza haraka, na hupakia kurasa za wavuti kwa kasi
- Ni nyepesi kuianzisha kutoka kwenye eneo-kazi lako
- Hupakia kurasa za wavuti mara moja
- Huendesha programu za wavuti haraka zaidi
2. Urahisi: Imeunda kwa ajili ya uthabati na urahisi wa matumizi
- Tafuta na uabiri hadi kurasa za wavuti kutoka kwenye kisanduku kimoja
- Panga na unadhifishe vichupo jinsi unavyotaka — haraka na kwa urahisi
- Fika kwenye tovuti uzipendazo kwa kubofya mara moja tu, kutoka kwenye vijipicha vya tovuti unazozitembelea zaidi kwenye ukurasa wa Kichupo Kipya
Mtindo: Mandhari ya kusisimua kivinjari chako
Tazama Onyesho la YouTube
kuhusu Mandhari ya Google Chrome kutoka kwa Wasanii.
Kwa maelezo zaidi kuhusu vipengele vya Google Chrome, tazama Kituo
cha Msaada cha Google Chrome.Kwa masasisho mapya zaidi, soma Blogu ya Google Chrome.
©2011 Google - Nyumbani Google - Kuhusu Google - Msaada - Sera ya faragha - Wasanidi tovuti - Programu huria
- Pakua
- Vipengele
- Sababu yetu ya kuunda kivinjari
- Sera ya faragha
- Programu
huria
Mtazamo mpya kwa kivinjari
Hapa Google, huwa tunatumia muda
wetu mwingi tukifanya kazi ndani ya kivinjari. Sisi hufanya utafutaji, kupiga
gumzo, kutuma barua pepe na kushirikiana katika kivinjari. Na kama nyinyi wote,
katika muda wetu wa ziada, huwa tunanunua vitu, kwenda benki, kusoma habari na
kuwasiliana na marafiki - yote kupitia kivinjari. Watu wanatumia muda zaidi na
zaidi kwenye wavuti, na wanafanya mambo ambayo hayakuwahi kudhaniwa wavuti
ulipojitokeza kama miaka 15 iliyopita.
Kwa sababu sisi hutumia muda mwingi
sana kwenye wavuti, tulianza kuwaza sana kuhusu kivinjari ambacho kingeweza
kuwepo ikiwa tungeanza kutoka mwanzo na kikiunda kwa kutumia sehemu bora zaidi
zilizokuwepo. Tulitambua kuwa wavuti ulikuwa umebadilika kutoka sana sana
kurasa rahisi za maandishi hadi programu anuwai na wasilianifu na kuwa tulihitaki
kukifikiria kivinjari upya kabisa. Tulichohitaji kilikuwa sio kivinjari tu,
bali jukwaa la kisasa la kurasa za wavuti na programu, na hicho ndicho
tulipanga kuunda.
Kijuu juu, tuliunda dirisha la
kivinjari la kisasa na rahisi. Kwa watu wengi, sio kivinjari kilicho cha
umuhimu. Ni zana tu ya kuendesha vitu vilivyo na umuhimi - kurasa, tovuti na
programu zinazounda wavuti. Kama ukurasa wa nyumbani wa Google, Google chrome
ni safi na nyepesi. Inakuondokea na kukufikisha unakotaka kwenda.
Chini ya chadarua, tuliweza kuunda
msingi wa kivinjari kinachoendesha programu wavuti za kisasa kwa njia bora
zaidi. Kwa kuweka kila kichupo katika "sanduku" pweke, tuliweza kuzia
kichupo kimoja kuzima kingine na kutoa ulinzi dhidi ya tovuti mbaya.
Tumeboresha kasi na mawasiliano katika sehemu zote. Pia tuliunda v8, injini ya
JavaScript yenye uwezo zaidi, kuendesha kizazi kijacho cha programu za wavuti
ambazo haziwezekani na vivinjari vya sasa.
Huu ndio mwanzo tu - mambo bado
kwenye Google Chrome. Tumezindua toleo hili la beta kwa ajili ya Windows ili
kuanzisha majadiliano mapana na tuwese kusikia kutoka kwako haraka
iwezekanavyo. Tunajitahidi kuunda matoleo ya Mac na Linux pia, na tutaendelea
kuifanya iwe nyepesi na yenye nguvu hata zaidi.
Tunawia deni kubwa kwa miradi mingi
ya programu huria, na tumejitolea kuendelea katika njia yao. Tumetumia sehemu
za WebKit ya Apple na Firefox ya Mozilla, na nyinginezo - na katika moyo huo,
tunafanya hati fumbo yetu iwe huria pia. Tunatazamia kushirikiana na jumuiya
yote ili kusaidia kuusukuma wavuti mbele.
Wavuti huimarika kwa chaguo na
uvumbuzi zaidi. Google Chrome ni chaguo lingine, na tunatumai kuwa itachangia
katika kuboresha wavuti hata zaidi.
Haya basi kutoka kwetu. Uhondo wa
Google Chrome ni uijaribu mwenyewe.
Post a Comment
Post a Comment