Ads (728x90)

HATIMAYE chama cha Wananchi CUF kimechukua uamuzi mgumu wa kumvua uanachama Mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohamed kwa kile kilichodaiwa kuwa ni njama zxa kumuangusha Katibu Mkuu wa chama hicho ambaye pia ni Makamu wa kwanza wa Rais Maalim Sef Sharif Hamad.

Kuvuliwa uanachama kwa Hamad kumeelezwa kuwa ni mwanzo wa kumong'onyoka kwa chama hicho ambacho awali kilionekana kuleta upinzani mkubwa kwa Chama tawala CCM na hivyo kitendo hicho ni kama kuanza kukimong'onyoa chama hicho.

Taarifa kutoka ndani ya kikao cha Baraza Kuu kilichoketi leo mjini Zanzibar zinaeleza kuwa Hamad ambaye pia aliwahi kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bugeni wakati huo chama hicho kikiwa na mvuto imemuondoa yeye pamoja na viongozi wengine watatu wanaoonekana kuchochea mapinduzi ya uongozi ndani ya chama hicho.





Post a Comment

Post a Comment