Dar es
salaam
Jitihada za
kutatua mgogoro na mgomo wa Madaktari nchini ambazo zilidhamiriwa kufanywa na Waziri
mkuu Mizengo Pinda leo zimegonga mwamba baada ya madaktari hao kugoma
kuhudhiuria kikao kilichoitishwa na Waziri Mkuu katika ukumbi wa Karimjee.
Hatua hiyo ya
Madaktari imehitimisha kile kilichoelezwa kuwa serikali bado imeshindwa kutatua
mgogoro wao wa muda mrefu na serikali kutosikiliza kilio cha wafanyakazi wa
sekta ya afya nchini.
Katika
ukumbi wa Karimjee ni baadhi ya watumishi wa taasisi za serikali pekee ndio
waliohudhuria ambapo hakuna hata Daktari mmoja aliyehudhuria hata mara baada ya
kuingia ukumbini Waziri Mkuu.
Kufuatia
kutotokea kwa madaktari hao ambao walitarajiwa kukutana na Waziri Mkuu ili
kusikiliza madai yao, Waziri Pinda alitangaza rasmi kuwa iwapo madaktari hao
watagoma kuingia kazini kesho siku ya Jumatatu watakuwa wamejiondoa wenyewe
katika utumishi wa umma.
‘’Madaktari
hawa tunawataka kesho waingie kazini iwapo watashindwa kufika kazini kesho
watakuwa wamejiondoa wenyewe kuwa watumishi wa umma’’alisema Bw. Pinda
Waziri Mkuu alitumia muda wake kuzungumza na
watumishi wa taasisi mbalimbali za serikali na kudai kuwa serikali itaingia
katika changamoto katika kipindi hiki cha mpito na kuwa hata hivyo bado
serikali inatoa fursa ya kukutana na madaktari hao kutafuta ufumbuzi wa madai
yao ambayo amedai kuwa ni ya msingi.
Post a Comment
Post a Comment