|
Madaktari wa JWTZ waanza kazi
Muhimbili
Dar
es salaam
MADAKTARI wa Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ) wameanza kutoa huduma ya matibabu katika Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) kukabiliana na upungufu wa madaktari uliosababishwa na mgomo unaoendelea.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa
Habari Dar es Salaam , Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Khajji Mponda
alisema madaktari hao wameanza kufanya kazi katika Hospitali hiyo kufuatia
maagizo ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyoyatoa juzi alipozungumza na vyombo
vya habari.
"Tumewaomba wenzetu kutoka
katika Jeshi letu ili kusaidia kutoa huduma za kitabibu kama Waziri Mkuu
alivyoagiza'' alisema Mponda.
Alisema madaktari 15 kutoka Jeshini
ndio walioanza kutoa matibabu katika Hospitali hiyo ili kukabiliana na uhaba
huo uliotokana na madaktari walioopo kwenye mafunzo kugoma.
Alisema madaktari hao wanafanya kazi
katika kitengo cha huduma za dharula kutokana na eneo hilo kudorora kwa huduma
na kuzidiwa na wagonjwa.
Alisema huduma za kitabibu
zinaendelea kama kawaida kufuatia baadhi waliokuwa kwenye mgomo kuendelea
kufanya kazi ingawa baadhi yao hasa wale walioopo kwenye mafunzo kuendelea na
mgomo huo.
Alisema madaktari waliorudi kazini
wamewasirisha madai yao serikali jambo ambalo ni zuri kuliko njia waliyokuwa
wanaitumia ya kugoma.
"Serikali ipo tayari kukutana
na madaktari hao hasa hao waliorudi kazini ilikufikia muafaka wa madai yao
lakini wale wanao lalamikia vichochoroni haitashughulika nayo'' aliongeza
Mponda.
Alisema mbali ya madaktari hao
kutoka jeshini wamepata madaktari wengine 80 kupitia programu mbalimbali za
Wizara yake na kwamba upungufu utakaojitokeza katika hospitali za mikoani
ambazo madaktari wao wapo kwenye mgomo huo ameagiza lishughulikiwe na Ofisi za
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali ya Mitaa (TAMISEMI).
"Kama itatokea kuwa na uhaba wa
madaktari katika hospitlai zilizopo mkoani tutawapatia madaktari lakini suala
hilo tumewaachia wenzetu kupitia TAMISEMI'' alisema Dk.Mponda.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Mifupa (M0I), Profesa Laurence Miseru alisema wameamua kusitisha huduma za
kliniki katika Hospitai hiyo ili kukabiliana na uhaba huo wa madaktari.
"Madaktari hao watafanya kazi
katika maeneo muhimu katika Hospitali ya Muhimbili na Taasisi ya Mifupa ya Moi
na kitengo cha magonjwa ya dharura'' alisema Miseru.
Aliongeza kuwa hivi sasa hali ya
matibabu kwenye hospitali hiyo imetengamaa ingawa katika baadhi ya wodi
kumekuwa hakuna wagonjwa.
Ametoa wito kwa wananchi kuondoa
wasiwasi waliokuwa nao kuwa katika hospitali hiyo hakuna matibabu kwamba wafike
kutibia baada ya huduma kuanza kutolewa.

STORI NA PICHA KWA HISANI YA DOTTO MWAIBALE WA JAMBO CONCEPT
Post a Comment
Post a Comment