Ads (728x90)

DEREVA ADEN Mwampyate(55) aliyepata ajali baada ya gari lake kugongwa anaendelea vizuri katika Hospitali Teule ya Ifisi iliyopo Halmashauri ya Mji wa Mbeya.

Mwampyate ambaye alitembelewa na MWANAFASIHI  kujua maendeleo yake alisema kuwa hivi sasa anaweza kufanya mazoezi kidogo kidogo ingawa mguu wake wa kulia bado unamsumbua.

Alisema kuwa baadhi ya ndugu zake walitaka kumhamisha kumpeleka Tumbi Kibaha lakini kutokana na huduma anazoendelea kupata katika Hospitali hiyo ameona bora aendelee kuhudumiwa hapo hadi hali yake itakapotengemaa.

Mwampyate ameenedelea kuwashukuru watu waliofika mara tu alipopata ajali na kuokoa maisha yake na kusema kuwa iwapo wasamaria wema hao wangechelewa angeweza kupoteza maisha kwa kupoteza damu nyingi.

''Tukio lililonitokea katika maisha yangu ni la kihistoria siwezi kusahau kamwe...namshukuru Mungu kwa kuwapa wasamaria wema moyo wa huruma wa kunisaidia hadi hivi nilivyo,''alisema Bw. Mwampyate.

Post a Comment

Post a Comment