KANISA MOJA
LA KIPENTEKOSTE LA MJINI MBEYA LIMEAMUA KUSARENDA MSAADA ULIOTAKIWA KUTOLEWA NA
KIGOGO MMOJA WA HAPA NCHINI KWA MASHARTI YA KUMKASHIFU MMOJA WA VIONGOZI MAHIRI
WALIOJIJENGEA HESHIMA NA SIFA KUBWA YA KUKUBALIKA HAPA NCHINI HUSUSANI KATIKA
MAPAMBANO DHIDI YA UFISADI.
KIGOGO HUYO
AMBAYE NI MMOJA WA VIONGOZI WENYE UWEZO MKUBWA WA KIFEDHA HAPA NCHINI INADAIWA
KUWA AMEANZA MCHAKATO WA KUWANIA URAIS MWAKA 2015 NA HIYO NI MOJA YA MBINU ZAKE
ZA MBIO ZA KUELEKEA IKULU MWAKA 2015.
TAARIFA ZA
KIUCHOKONOZI AMBAZO ZIMEJAA KATIKA DAWATI HILI LA MWANAFASIHI ZIMETANABAHISHA
KUWA MPANGO HUO WA KUENEZA KASHFA DHIDI
YA KIONGOZI ANAYEHESHIMIWA MKOANI MBEYA NA TANZANIA ZIMEPANGWA ILI KUWEKA NJIA
YA KUKUBALIKA KUTOKANA NA KASHFA AMBAZO ZIMEKUWA ZIKIELEZWA KUWA KIGOGO HUYO
ANAHUSIKA KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE JUU YA TUHUMA ZA UFISADI.
AIDHA MARA
BAADA YA TAARIFA ZA KUHITAJIWA KWA KIGOGO HUYO KUJA KUCHANGIA HARAMBEE YA
KANISA ILIDAIWA KUWA ALITOA MASHARTI YA KUANDAA MABANGO YATAKAYOSAMBAZWA MJI
MZIMA YAKIELEZEA UBAYA WA KIONGOZI ANAYEHESHIMIWA IKIWEMO KUENEZA UZUSHI JUU YA AFYA YAKE.
TAARIFA
ZAIDI ZINAELEZA KUWA BAADHI YA MARIPOTA WAMEKUWA WAKITUMIKA KWA NAMNA MOJA AMA
NYINGINE KUANDAA NJIA NYEUPE YA KUPITA KIGOGO HUYO KWA KURIPOTI KILA JEMA
LINALOFANYWA NA KIGOGO HUYO,HATA KAMA JEMA HILO NI DOGO KAMA SISIMIZI.
Post a Comment
Post a Comment