Tanzania Film Critics Association ni mradi ulio
chini ya Image Profession wenye kuhusisha kundi la wanachama wa hiyari kwa
malengo ya kuleta changamoto za kimaendeleo katika Tasnia ya Filamu ikiwa
pamoja na kuchambua,kukosoa,kushauri na kusaidia maswala mazima yahusuyo Filamu
na wahusika wa Filamu hapa Tanzania.
Pamoja na kufanya shughuli zake kwa kutumia
mitandao ya kijamii ,kundi pia litakuwa na shughuli zitakazofanyika katika
mazingira mbali mbali ya kawaida ikiwa pamoja na kuwa na mabaraza
yatakayohusisha wataalamu mbalimbali wa Tasnia ya Filamu.
Waliopendekezwa watakaoungana na wajumbe watatu
kutoka Image Profession(IP)kuingia katika kamati ya watu kumi itakayosimamia na
kuratibu utendaji wa Tanzania Film Critics Association,katika kipindi cha miezi
sita mpaka mwaka.
Wafuatao ni wajumbe saba
na idadi ya mapendekezo waliyoyapata kutoka katika mchakato wa
kupendekeza uliofanyika kwenye kundi hili kwenye mtandao wa kijamii wa
Facebook.
1.
John Kitime (47)
2.
Goddy Semwaiko (37)
3.
Bishop Hiluka (36)
4.
Apilike Gordon (33)
5.
Rashid Faraji (31)
6.
Rashid Adam (25)
7.
Richard Mloka (24)
Mkutano wa kwanza wa wajumbe wakamati utakuwa siku
ya Jumamosi ya Tarehe 11.02.2012 ,tunatoa shukrani kwa kila mmoja aliyeshiriki
katika mchakato mzima wa kundi na wale wote wanaochukuwa muda wao kutoa mada
mbalimbali kuchangia na hata kusoma yale yanayoandikwa kwenye kundi..
Post a Comment
Post a Comment