-Wanyimwa chakula cha usiku
-Walazimishwa kufua nguo za ndani na kuosha vyombo
NAIROBI,Kenya
WANAUME
katika miji ya mikoa ya Kati na Nairobi nchini Kenya wamedhamiria kuitisha mgomo wa kula kwa juma
zima kwa kile walichosema kupinga kitendo cha Kupigwa na wake zao.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Wanaume nchini Kenya Nderutu Njoka amesema kuwa wanawake hao wamekuwa na tabia ya kuwapiga wanaume na kuwanyanyasa kupita kiasi ikiwemo kuwanyima ‘chakula cha usiku’ hali inayofanya wakose raha.
‘’Tumeazimia
kugoma kula majumbani mwetu kwa juma moja kushinikiza wanawake kuacha vitendo
vya kuwapiga wanaume zao..wanawake wanafanya unyanyasaji dhidi ya
wanaume,;;anasema Bw. Njoka.
Hata hivyo
kwa upande wa wanawake nchini humo wamedai kuwa,wanaaume wengi hususani katika
mikoa ya Kati Na Nairobi nchini Kenya wamekuwa ni sawa na ‘wanaume suruali’wamekuwa
wakiishi kwakuwategemea wanawake badala ya kujishughulisha na utafutaji wa
riziki.
‘’Wanaume
pande za hapa kwetu wamekuwa ni ‘’Wanaume Suruali’ hawako na mbinu za kujua
kutafuta chapaa ndio maana wanakutwa na Kipigo cha mara kwa mara’’ alisema
mwanamke huyo mkazi wa mkoa wa Kati.
Imedaiwa kuwa
takribani wanaume 500,000 wamekuwa wakikumbwa na vipigo kutoka kwa wanawake zao
ikiwemo kuwanyima ‘Chakula cha Usiku’kuwalazimisha
kufua nguo za ndani na kuosha vyombo ambapo hata katika kulala hulazimika
kulala ‘Mzungu wa Nne’na wanaume wanapohitaji kustarehe na wake zao hupigwa
Kipepsi.
(Kwa msaada wa BBC
SWAHILI)
Post a Comment
Post a Comment