CCM
isiwatishe kujiunga CHADEMA
Na Peter Mwenda,Dar es salaam.
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Temeke kimewataka wananchi wasikubali vitisho vinavyotolewa wakati wakijiunga chama hicho kwani hiyo ni demokrasia ya kila mtanzania.
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Temeke, Bw. Stephano Warioba akizungumza na wananchi wa Gezaulole jana alisema wananchi wengi wamekuwa wakitishika kujiunga CHADEMA kutokana na vitisho wanavyopata kuwa watatengwa na kufanya Chama cha Mapinduzi kuzoa wanachama ambao hawana mapenzi na chama hicho.
"Msikubali kudanganywa kujiunga chama cha upinzani cha CHADEMA hayo ni matakwa ya mtu mwenyewe na si Serikali wala CCM" alisema Bw. Warioba wakati wa ufunguzi wa tawi la Nelson Mandela la Gezaulole, Kigamboni.
Awali Diwani wa Viti maalum Jimbo la Kawe, Bibi Angela Sawaya aliwataka wanawake waache woga badala yake wajiunge Chadema kukomboa jamii ambayo alisema inashindia mlo mmoja kwa siku.
Bibi Sawaya alisema wanawake ndiyo walezi wa familia hivyo ili kuondokana na taabu wanazozipata za kukosa huduma muhimu ni lazima wajiondoe huko waliko wajiunge Chadema.
Katika hafla hiyo mlezi wa tawi la Gezaulole,Bw. Paulo Mpema na mwanae John walitunukiwa cheti cha uvumilivu katika tawi hilo ambao waliwahi kubaki wawili pekee baada ya wengine kukihama chama hicho.
Katika hatua nyingine Chadema kimesema kitahikisha wananchi wake wote wanapata huduma muhimu za umeme, maji, zahanati na barabara katika wilaya ya Temeke. (Stori kwa hisani ya Mwenda Blog)

Post a Comment
Post a Comment