Ads (728x90)

MBUNGE wa Monduli Bw. Edward Lowassa leo mchana amemwaga jumla ya sh. milioni kumi katika kanisa la EAGT kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo mjini Tunduma.




Bw. Lowassa ambaye alikuwa akikimbizana na muda aliamua kuondoa udhia kwa kusimama moja kwa moja jukwaani wakati baadhi ya waumini wakitoa ahadi za kuchangia fedha za ujenzi wa kanisa hilo na kusema kuwa anawaomba radhi waumini wa kanisa hilo na kisha akatoa kitita cha fedha zilizofungwa na bahasha ya kaki na kumkabidhi Askofu wa kanisa hilo Keneth Kasunga.

Post a Comment

Post a Comment