Ads (728x90)




Huyu ndo mdogo wake Kanumba akìhojiwa ambapo amekiri kuwa Lulu alikuja nyumban na kuingia chumbani kwa kaka yake baadaye alisikia majibizano na kisha Lulu alitoka nje na kumueleza mdogo wake kuwa kaka yake ameanguka chini, aliingia ndani na kumkuta amelala chini, aliporudi sebuleni Lulu alikuwa ametoweka.(picha hii na   Caption yake ni kwa hisani ya www.spotistarehe.wordpress.com








Yaelezwa chanzo cha kifo chake kilitokana na ugomvi ulioibuka nyumbani kwake,wasanii maarufu walifurika nyumbani kwake kushuhudia kifo hicho,majira ya saa tisa usiku kundi la wasanii wenzake walifika nyumbani na kuangalia kilichotokea na kufikwa na simanzi nyumbani kwake Sinza mwili wake ulichukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili.

Aidha taarifa zaidi zinaeleza kuwa Mpenzi wake Lulu ambaye pia ni msanii chipukizi wa maigizo alitoka nje na kumueleza mdogo wake Kanumba kuwa kaka yake ameanguka ndani, mara alipoingia ndani akamkuta kaka yake akiwa ameanguka chini akiwa amefariki dunia.

Post a Comment

Post a Comment