Ads (728x90)

Taarifa zilizotujia kupitia kituo cha Matangazo cha BBC na radio mbalimbali za nchini Malawi zimeeleza kuwa Rais Bingu wa Mutharika(78) amefariki dunia kutokana na shinikizo la moyo.

Inaelezwa kuwa Rais Mutharika amefariki dunia akiwa njiani kupelekwa nchini Afrika Kusini ambako alitakiwa kupata matibabu ya kina juu ya matatizo yake yaliyomkuta.


Historia yake kwa ufupi


Hayati Bingu wa Mutharika amezaliwa kwa baba Ryson Webster Thom Februari 24 1934 katika kijiji cha Thyolo, mama na baba yake Eleni Thom Mutharika wote walikuwa ni wanachama wa kanisa la Church Of Scotland Mission ambalo baadaye likaitwa CCAP, baba yake alikuwa mwalimu kwa miaka 37.

Amemaliza elimu yake ya msingi mjini Blantyre na baadaye alipata shahada ya daraja la A Cambridge kati ya mwaka 1956,ambapo mwaka 1964 alikuwa ni mmoja kati ya wamalawi 32 waliochaguliwa na Hayati Hasting Kamuzu Banda aliyekuwa rais wa Malawi kati ya 1961-1964 kuelekea nchini India kwa nafasi iliyotolewa na Waziri Mkuu wa India Bibi Indira Gandhi kwa ajili kupata diploma.

Hayati Mutharika alimuoa Bi.Ethel Zvauya  ambaye ni raia wa nchini Zimbabwe ana kupata watoto wanne,kwa bahati mbaya mkewe alifariki kwa ugonjwa wa kansa Maye 28 2007, baadaye mwaka Mei Mosi 2010 Hayati Mutharika alitangaza kumuona Waziri wa zamani wa Utalii Bi. Callista Chimombo.

Hayati Mutharika ana kaka yake anaitwa Peter Mutharika ambaye ni mhadhiri katika chuo Kikuu cha Washington kilichopo St. Louis. Mwaka 2009 alichaguliwa kuwa Mbunge na baadaye kuchaguliwa katika Baraza la Mawaziri wa nchini humo na kuwa Waziri wa Sheria.

Post a Comment

Post a Comment