SERIKALI mkoani Mbeya, imeshangazwa na kitendo cha Mkuu wa
Wilaya ya Mbozi Bw. Gabriel Kimolo kutangaza hadharani juu ya kujiuzulu kwake
ilhali alikuwa akijua wazi kuwa hayumo katika orodha ya wakuu wa wilaya wapya
watakaoteuliwa na Rais.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo alasiri
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro
kuwa kitendo cha Mkuu huyo kutumia vyombo vya habari kutangaza kujiuzulu
ni kujikosha kwa jamii kwani anajua wazi kuwa hayumo ndani ya orodha ya wakuu
wa wilaya wapya.
Bw. Kandoro alisema
kuwa Mkuu huyo wa wilaya alimfuata ofisini kwake Machi 24 na kumueleza kuwa
amepata taarifa za kutokuwemo katika orodha ya wakuu wa wilaya wapya hivyo
anashangazwa na kitendo hicho kwani anaamini hakupaswa kujiweka hadharani na
kulaumu makampuni.
Alisema kuwa
kulingana na taarifa za Mkuu huyo ni kwamba alifika ofisini kwake na kumueleza
kuwa alipata taarufa hizo Machi 23 kutoka katika idara inayohusika kwamba jina
lake halimo.
Bw.Kandoro alisema kuwa katika maelezo yake mkuu huyo alikuwa
akilalamika kwanini ameachwa wakati yeye ni mtendaji mzuri kwa wilaya na Taifa.
Alisema kuwa alichokifanya ni kujikosha kwa jamii ili
isishangae wakati uteuzi mpya wa wakuu wa wilaya utakapotangazwa na kwamba Bw.
Kimolo hakupaswa kuyatupia lawama na
kwamba anapaswa kukubali matokeo ili aweze kuondoka kwa amani.
Kadhjalika alimtaka kuacha kuyapaka mayope baadhi ya
makampuni kwamba yamehusika kwa namna moja ama nyingine juu ya kudorora kwake
kuhusu utendaji wake kudorora.
Post a Comment
Post a Comment