MWANDISHI wa
Kampuni ya Business Times inayochapisha gazeti la MAJIRA mwakilishi wa mkoa wa
Mbeya Bw. Charles Mwakipesile amekuwa ni miongoni mwa wagombea 24 waliojitokeza
kuchukua fomu katika ofisi ya CCM wilaya ya Mbeya mjini kuwania nafasi za
Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa.
Bw.
Mwakipesile ambaye alikuwa ameambatana na Katibu mwenezi wa CCM Kata ya Itiji
Bw. Livingstone Mwakapesa na Katibu wa CCM kata ya Mwakibete Bw.George Mapunda
amerudisha fomu hiyo mbele ya Katibu wa CCM wilaya ya Mbeya Bw.Raymond
Mwangwala na kusema kuwa ameamua kujitosa katika siasa kuleta changamoto kwa
vijana.
Amesema kuwa
CCM ni chama kikongwe ambacho kikipata viongozi vijana kinaweza kurekebisha
dosari ndogondogo zinazojitokeza ambazo ni changamoto zinazotokana na kukua kwa
demokrasia ya vyama vingi nchini.
Amesema ili
kukabiliana na changamoto chama kinahitaji kuwa na nguvu kubwa ya vijana ambao
anaamini kwa kushirikiana na busara za wazee kinaweza kupiga hatua hasa
kutokana na historia yake ya kuongoza kwa amani, utulivu kwa zaidi ya miaka 40.
Akizungumza
wakati akipokea fomu hiyo Katibu wa CCM wilaya ya Mbeya Bw.Mwangwala amesema
kuwa amefurahi kuona vijana wamejitokeza kwa wingi kuchukua fomu na kwamba hadi
sasa jumla ya wanachama 24 wamejitokeza kuchukua fomu na kurejesha jana mchana.
Bw.
Mwangwala amesema kuwa kila mwanachama anayo haki ya msingi kugombea nafasi
yoyote ya uongozi kwa nia ya kuleta changamoto ndani na nje ya chama.
Post a Comment
Post a Comment