TAARIFA ZIMEELEZA KUWA MKUTANO HUO WA CCM HAUKUWA NA MVUTO KAMA ULE WA CHADEMA NA KWAMBA KITENDO KIMEZIDI KUONESHA UDHAIFU KWA CHAMA HICHO KIKONGWE NCHINI AMBACHO KWA KADRI SIKU ZINAVYOKWENDA KINAONESHA DALILI YA KUPOTEZA MVUTO.
AIDHA IMEELEZWA KUWA JITIHADA ZA KUKIONUSURU CHAMA HICHO KIKO MIKONONI MWA VIJANA NA BAADHI YA MAWAZIRI WAWAJIBIKAJI AMBAO ANGALAU WANAONESHA DALILI ZA KUKUBALIKA KWA WANANCHI NA KWAMBAA HATA HIVYO MGAWANYIKO ULIOPO BAINA YA VIONGOZI NDANI YA CCM IMEKUWA NI SUMU INAYOMEA SIKU HADI SIKU KIASI CHA KUWAFANYA VIONGOZI WAKUU WAKIWEMO MARAIS WASTAAFU MZEE RUKSA NA BW. MKAPA KUOGOPA KUKAA PEMBENI KWA KUOGOPA KUCHAFULIWA MAJUKWAANI.
TAARIFA ZINAELEZA ZAIDI KUNDI KUBWA LINALOONEKANA KUTEKA HADHIRA YA WANANCHI KWA SASA NI LILE LINALOMKUBALI WAZIRI MKUU MSTAAFU, EDWARD LOWASSA AMBAPO KWA KUTUMIA UKARIBU WAKE NA JAMII YENYE MAHITAJI KUPITIA MICHANGO YAKE YA MAMILIONI KWENYE NYUMBA ZA IBADA IMEKUWA NI MWIBA MCHUNGU KWA CCM HUSUSANI PALE INAPOELEZWA KUWA KUJIUZULU KWA LOWASSA NI SAWA NA MBUZI ALIYETOLEWA KAFARA KULINDA MASLAHI YA WAKUBWA WALIOKO SERIKALINI.
Post a Comment
Post a Comment