Ads (728x90)

OFISI YA KAMANDA WA POLISI WILAYANI MBOZI OCD IMETEKETEZWA KWA MOTO NA WATU WASIO FAHAMIKA MWISHONI MWA WIKI ILIYOPITA AMBAPO NYARAKA MUHIMU ZILIZOMO NDANI YA KOMPYUTA NA ZILE ZILIZOHIFADHIWA KATIKA MAFAILI ZIKIWA NI KATI YA ZILIZOHARIBIWA KWA MOTO.

TAARIFA RASMI ZA KUTEKETEZWA KWA NYARAKA HIZO ZILIUFIKIA MTANDAO HUU AMBAPO MTOA TAARIFA ALIDAI KUWA ZIPO BAADHI YA NYARAKA MUHIMU ZA KIUTENDAJI ZIKIWEMO ZINAZOHUSU KESI MBALIMBALI ZILIZOPO KATIKA HATUA YA AWALI YA UPELELEZI AMBAZO ZIMETEKETEA KWA MOTO.

HATA HIVYO MOTO HUO ULIONEKANA ZAIDI KUSHAMBULIA NYARAKA HUKU JENGO LA OFISI HIYO YA OCD IKIONEKANA KUTOATHIRIWA NA MOTO HUO.

Post a Comment

Post a Comment