KUFUATIA AJALI ILIYOTOKEA JANA NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU 10 NA KUJERUHI WENGINE 25, HALI YA MBUNGE WA MBEYA VITI MAALUMU CCM, MARY MWANJELWA INAENDELEA VIZURI.
DKT. MWANJELWA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI AMBAPO ALIONEKANA AKIZUNGUMZA VYEMA KWA UFASAHA NA KUWATAMBUA WATU WANAOINGIA NA KUTOKA.
''HALI YANGU NI NZURI NAJISIKIA MAUMIVU SEHEMU ZA KIUNONI NA MBAVU LAKINI NAJISIKIA VIZURI''ALISEMA DKT.MWANJELWA.
NJE YA WODI ALIYOLAZWA KULIKUWA NA BAADHI YA VIONGOZI WA CHAMA AKIWEMO MBUNGE MWENZIE WA VITI MAALUMU, BI. HILDA NGOYE NA MWENYEKITI WA UWT MKOA BI. FROLENCE KYENDESYA AMBAO NAO WALIFIKA KUMJULIA HALI.
|
MBUNGE WA VITI MAALUM MBEYA DKT.MARY MANJELWA AKIWA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA IFISI MARA BAADA YA GARI YAKE KUTEKETEA KWA MOTO JANA. |
|
HIVI NDIVYO ILIVYO GARI YA DKT. MARY MWANJELWA BAADA YA KUTEKETEA KWA MOTO. |
|
TENKI LA MAFUTA LIKITEKETEA KWA MOTO MARA BAADA YA KUGONGA GARI TATU NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU KUMI NA MAJERUHI 25 ENEO LA MBALIZI JANA. |
|
MBUNGE WA VITI MAALUM MKOA WA MBEYA BI.HILDA NGOYE AKIWAFARIJI NDUGU NA JAMAA WA DKT. MWANJELWA BAADA YA KUMUONA WODINI. |
|
MWENYEKITI WA UWT MKOA MBEYA BI FROLENCE KYENDESYA AKITOKA HOSPITALI KUMTEMBELEA DKT. MWANJELWA ALIYELAZWA HOSPITALI YA IFISI. |
|
|
|
|
|
AIDHA NJE YA WODI HIYO WALIKUWEPO BAADHI YA VIONGOZI WA CCM AMBAO WALIKUWA WAKIWADHIBITI WATU KUTOMWELEZA MBUNGE HUYO KUWA MMOJA WA WATU WALIOKUFA KATIKA AJALI HIYO NI KATIBU WAKE AMINA MWAMPASHI AMBAAAYE ALITEKETEA KWA MOTO NA DEREVA WAKE ALIYEJERUHIWA NA KULAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MBEYA.
Post a Comment
Post a Comment