Ads (728x90)


SIKU  moja baada ya chama cha Demokrasia na maendeleo mkoani Mbeya kubeza viongozi w CCM mkoa wa Mbeya waliochaguliwa kuwa ni  legelege Mjumbe Halmashauri Kuu ya CCM Taifa mkoa wa Mbeya Bw. Sambwee Shitambala amebeza kauli hizo na kuahidi kuimaliza CHADEMA mkoani humo.
Shitambala ambaye aliwaqhi kuwa Mwenyekiti wa mkoa wa CHADEMA alisema kuwa anajua mbinu zote za kuimaliza CHADEMA na kwamba wasitarajie kutetea nafasi za ubunge zilizopatikana chini ya uongozi wake kuwa zitaendelea kubaki mikononi mwa CHADEMA.
Alisema kuwa viongozi wote wa CHADEMA waliopo wamepitia mikononi mwake na amekuwa akijua udhaifu wao wa uongozi hivyo atatumia fursa hiyo kukimaliza kabisa CHADEMA mkoani humo na amedhamiria kuijenga CCM mpya  yenye tija na maslahi kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya.
‘’Niliijenga CHADEMA kwa mikono yangu na sasa nitaibomoa kwa mikono yangu, hawana mbinu mbadala za kiuongozi, wote waliopo ni wababaishaji tu,’’alisema Shitambala.

Miongoni mwa udhaifu ambao Shitambala anaueleza ni pamoja na viongozi waliopo kushindwa kutekeleza ahadi walizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2010 na kuwa mengi wanayoyafanya hayana maslahi kwa wananchi na Taifa.

Alisema kuwa kutokana na kuwa mpiganaji na msomi wa sheria alishangaa kuona viongozi hao ambao wengi wao ameshiriki kuwapa ubunge wakigeuza ajenda na kuamua kuanzisha maandamano nchi nzima na kutoka nje bungeni wakati Rais Kikwete akihutubia hali ambayo alisema ni utovu mkubwa wa nidhamu.


Alisema kuwa CHADEMA ni chama chenye watu wasioweza kufikiri kwa haraka kutokana na ukweli kuwa Watanzania wanazo akili za kutosha kujitambua na kutoyumbishwa wala kuamuliwa juu ya amani ya nchi yao.

Post a Comment

Post a Comment