Na, Rashid
Mkwinda,
MAMA wa mtoto
Aneth Johanes aliyefanyiwa unyama na hatimaye kukatwa mkono Asera Mkandara amewasili Jijini Mbeya na kutoa shukurani kwa
wananchi na majirani waliosaidia kutoa taarifa na hatimaye kuokoa maisha ya
mwanaye aliyekuwa akiishi kwa mateso.
Bi. Mkandara
alizungumza hayo alipotembelewa na wanahabari waliofika wodi namba 8 kumjulia
hali mtoto Aneth na kusema kuwa alipewa taarifa za kutokea kwa matatizo ya
mwanaye lakini hakufafanuliwa ni tatizo gani alilopata.
Anasema kuwa
amewasili Jijini Mbeya akitokea kwao Muleba Bukoba na kumkuta mwanaye Aneth
ambaye ni mtoto wake wa pili baada ya mwanaye wa kwanza mwenye umri wa miaka 7
anayelelewa na bibi yake mjini Bukoba.
Anasema kuwa
hata hivyo yeye hana shughuli maalumu zinazomuendeshea maisha yake isipokuwa
biashara ndogo ndogo hivyo kuchukuliwa kwa mtoto wake na kaka yake aliyemtambulisha
kwa jina moja la Mkandara ilikuwa ni sehemu ya msaada kwake.
Mama huyo
anafafanua kuwa anashukuru kukuta mwanaye ni mzima na anawashukuru madaktari
waliompa msaada kwani inawezekana huduma za matibabu zingechelewa angeweza
kupata madhara makubwa.
Anasema kuwa
kwa sasa anasaidia na ndugu na majirani na baadhi ya watu wanaomiminika
hospitalini hapo kutoa msaada.
YEYOTE
MWENYE MAPENZI MEMA ANAWEZA KUTOA MSAADA KUPITIA NAMBA YA SIMU YA MKONONI YA
MAMA HUYO 0756-293784
|
Post a Comment
Post a Comment