MTOTO ANETHY JOHANES AKIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA WODI NAMBA 8 ANAKOPATIWA MATIBABU MTOTO HUYO ALIFIKISHWA HAPO BAADA YA MAMA YAKE MDOGO KUMCHOMA MOTO HUKU AKIMLISHA KINYESI AMBAPO BAADAYE WASAMARIA WEMA WALIJITOKEZA KUMUOKOA MTOTO HUYO NA BAADAYE KUMPELEKA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA .HATA HIVYO MARA BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALINI HAPO MADAKTARI WALILAZIMIKA KUMKATA MKONO WAKE BAADA YA KILE KINACHODAIWA KUWA ANGEWEZA KUPATA MADHARA ZAIDI KWA KUWA MKONO WAKE ULIANZA KUOZA.KWA MUJIBU WA MUUGUZI WA WODI HIYO AMBAYE HAKUTAKA KUTAJWA JINA LAKE KWA KUWA SI MSEMAJI, ALISEMA KUWA HIVI SASA MTOTO HUYO YUKO CHINI YA UANGALIZI WA HOSITALI HIYO ANAHUDUMIWA MATIBABU NA KUPEA CHAKULA AMBAPO ANAPATIWA YAI MOJA NA KARANGA MAALUMU NYAKATI ZA ASUBUHI PAMOJA NA CHAKULA. |
|
|
Post a Comment
Post a Comment