MSANII maarufu wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amepata
dhamana leo baada ya kukidhi masharti aliyowekewa na mahakama.
Dhamana hiyo imetolewa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada
ya hoja za mawakili wanaomtetea kukubalika.
Masharti aliyokuwa amepewa ni pamoja na wadhamini wawili wafanyakazi wa
serikali wenye kiasi cha Sh. milioni 20 kila mmoja na kuwasilisha pasi ya
kusafiri ya msanii ili kutotoka nje ya nchi hadi kesi hiyo itakapokamilika.
Huku mashabiki wake na baadhi ya wasnii wenzake wakiwa na furaha
mahakamani hapo, kila mmoja alisikika akisema Mungu mkubwa.(CHANZO GLOBAL
PUBLISHERS)
|
Post a Comment
Post a Comment