Ads (728x90)


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
PRESS RELEASE” TAREHE 14.01.2013.

WILAYA YA MOMBA – MAUAJI
  
MNAMO TAREHE 13.01.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KALUNGU KIJIJI CHA IVUNA TARAFA YA KAMSAMBA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. WATU WAWILI AMBAO NI 1.ERNEST S/O TWINI MOLELA NA MIZINARA D/O MILILO @ MATELA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IVUNA WALIUAWA KWA KUPIGWA NA WATU WASIOFAHAMIKA KISHA KUWAZIKA KATIKA KABURI MOJA . CHANZO NI TUHUMA ZA KISHIRIKINA BAADA YA MAREHEMU HAO KUTUHUMIWA KUWA NI WACHAWI KWA KUMLOGA MAREHEMU NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA ALIYEFARIKI DUNIA TAREHE 12.01.2013 MAJIRA YA SA 16:00HRS BAADA YA KUUGUA MUDA MREFU. TUKIO HILO LILITOKEA WAKATI WA MAZISHI YA MAREHEMU NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA AMBAPO KUNDI LA WATU WASIOPUNGUA KUMI WALIPANDISHA HASIRA NA KUWATUHUMU MAREHEMU HAO KUHUSIKA NA KIFO CHA NDUGU YAO NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA HIVYO KUANZA KUWASHAMBULIA KWA KUTUMIA NGUMI, FIMBO NA MAWE KISHA KUWATUMBUKIZA KATIKA KABURI ALILOKUWA AKIZIKWA MAREHEMU NONGWA S/O HUSSEIN MOLELA WAKIWA HAI NA KUWAZIKA WOTE WATATU KATIKA KABURI HILO MOJA. BAADA YA HAPO WATU HAO WALIKWENDA NYUMBANI KWA ERNEST S/O TWINI MOLELA NA KUICHOMA MOTO NYUMBA YAKE. KUFUATIA TUKIO HILO WATUHUMIWA WAWILI WALIOKUWA VINARA WA TUKIO HILO WAMEKAMATWA AMBAO NI 1. VENA S/O ERNEST MOLELA [MTOTO WA MAREHEMU ERNEST S/O TWINI MOLELA], MIAKA 26, MUWANDA, MKULIMA NA 2. EMANUEL S/O CHRISTOPHA, MIAKA 16, MUWANDA MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IVUNA.  MAREHEMU WOTE WATATU NI NDUGU WA UKOO MMOJA. TARATIBU ZA KUFUKUA KABURI ILI MIILI YA MAREHEMU IFANYIWE UCHUNGUZI ZINAFANYWA. AIDHA TARATIBU ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAFIKISHWE MAHAKAMANI.KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA  WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAHESHIMU NA KUTII SHERIA PASIPO KUSHURUTISHWA. PIA ANAIASA JAMII KUACHANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KWA JAMII IKIWA NI PAMOJA NA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO. AIDHA ANATOA RAI KWA JAMII/KIKUNDI CHA WATU WENYE KERO/MALALAMIKO,USHAURI ,UJUMBE MAALUM KUTAFUTA NJIA ILIYO HALALI KUFIKISHA KERO,MALALAMIKO,USHAURI ,UJUMBE WAO KWA NJIA YA MAZUNGUMZO BADALA YA KUTUMIA VURUGU/FUJO NA KUSABABISHA MAUAJI.

Post a Comment

Post a Comment