| Add c 
CHAMA
 cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kuanzia sasa hakitakubali 
kuwapokea mamluki kutoka CCM ambao hutumwa kwa ajili ya kukivuruga chama
 hicho. 
Kauli
 hiyo imetolewa leo mchana na Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Freeman 
Mbowe alipokuwa akizungumza na wanachama na wajumbe wa chama hicho 
kwenye uzinduzi wa Baraza la Uongozi Kanda ya Nyanda za Juu Kusini. 
Bw. 
Mbowe amesema kuwa kundi la mamluki wanaotumwa kwa ajili ya kuvuruga 
upinzani halina nafasi ndani ya chama hicho kwa sasa na kwamba chama 
hicho hakitaendelea kuwavumilia wala kuwapokea mamluki hao. 
Amesema kuwa 
CHADEMA haitapokea tena mamluki na kutoa onyo kwa viongozi waliopo ndani
 ya chama hicho kutotanguliza maslahi yao binafsi  badala ya maslahi ya 
nchi.Amesema migogoro mingi ya kisiasa ndani ya vyama vya upinzani 
inasababishwa na kupandikiziwa wanachama wasio waaminifu na waadilifu 
ambao nia yao ni kuvitengenezea migogoro vyama vyote vinavyokubalika na 
wananchi. 
Amesisitiza
 kuwa yeye kama Mwenyekiti wa Chama Taifa hatokubali kuiona hali hiyo 
kwa kuwa gharama ya kurejesha heshima ya chama inaweza kuchukua hadi 
miaka 20.Alitolea mfano vyama vya NCCR-Mageuzi na CUF ambavyo vilikuwa 
na nguvu kubwa na kwamba vyama hivyo kwa sasa vimekosa mvuto kwa 
wananchi hali ambayo itavichukua muda mrefu kurejesha heshima yake. 
 
aption
 | 
Post a Comment