Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimjulia hali Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, ambaye pia ni Mhariri
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda,
aliyelazwa katika Wodi ya Moi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, baada
ya kujeruhiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wakati
akiingia nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mkurugenzi wa Gazeti la Mwana Halisi, Said Kubenea.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri, ambaye pia ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda, akionekana jinsi
alivyojeruhiwa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimjulia hali Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, ambaye pia ni Mhariri
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda,
aliyelazwa katika Wodi ya Moi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, baada
ya kujeruhiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wakati
akiingia nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPP Regnard Mengi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimjulia hali Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, ambaye pia ni Mhariri
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Absalom Kibanda,
aliyelazwa katika Wodi ya Moi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, baada
ya kujeruhiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo wakati
akiingia nyumbani kwake maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
*******************************
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri na Mhariri Mkuu wa Mtendaji wa Kampuni ya New
Habari 2006, wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Dimba, Bingwa na
Dimba, Absalom Kibanda, amevamiwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia
leo akiwa ndani ya gari lake wakati akiingia nyumbani kwake maeneo ya
Mbezi-Beach, jijini Dar es Salaam.
Akielezea tukio
hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya New Habari, Hussein Bashe
amesema Kibanda alivamiwa majira ya saa sita usiku wa jana, akitokea
kwenye majukumu yake ya kila siku. Inadaiwa kuwa alitolewa kwenye gari,
akapigwa kichwani, akajeruhiwa jichoni na kisha kutelekezwa mbali kidogo
ya nyumbani kwake.
Baada
ya tukio hilo, wasamaria wema waliomwona walimpeleka katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili, ambako alipokelewa vizuri na madaktari na
kumpatia tiba ya awali na baadaye kumhamishia kwenye Taasisi ya Tiba ya
Mifupa (MOI) ambako mpaka sasa anaendelea na matibabu.
Watu waliotenda ukatili huo hawakuchukua kitu chochote kwenye gari.
Kwa
mujibu wa maelezo ya mgonjwa aliyekaririwa akizungumza kwa shida,
ameeleza kuwa, majira ya usiku wakati akiingia nyumbani kwake alivamiwa
na watu watatu --mmoja akiwa ameshika bastola na wawili wakiwa wameshika
nondo-- ambapo alipofika nje ya nyumba yake, watu hao walilivamia gari
lake na kuvunja mlango wa gari lake, wakamtoa nje, wakaanza
kumshambulia, wakamtoa meno mawili, wakamng'oa kucha katika moja ya
vidole vyake na kumtoboa jicho lake kwa nondo.
Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto, alisema kuwa watu hao waliohusika wakamatwe ili sheria ichukue mkondo wake.
''Tusingependa kama waandishi kuamini yanayosemwa lakini kutokana na uadilifu mkubwa wa vyombo vyetu vya ulinzi na Usalama kuwapata watu ambao wamehusika na tukio hilo.
Sisi tunaamini tukio hili la mwenzetu kuvamiwa na watu hao halikuwa kwa bahati mbaya ni Jambo ambalo linaonekana Kama limepangwa na Kama ni hivyo lengo na madhumuni yake ni nini kwa waandishi wa Tanzania? Uhuru na Usalama wa waandishi upo wapi?Kutakana na tukio hili la mpiganaji na Kiongozi wetu kuvamiwa ,ipo haja ya sisi waandishi kuungana pamoja katika kutafuta Usalama wetu. Kuna matukio mengi ya waandishi yametokea na tumekuwa tukipiga kelele lakini matokeo yake hakuna hatua ambazo serikali inayafanyia kazi.Kutokana na majeraha makubwa aliyopata mwenzetu, tunaiomba serikali na hasa Mheshimiwa Rais, Dr. Jakaya Kikwete kutoa Msaada wa mwenzetu kwenda kutibiwa nje,tunaamini serikali ni sikivu na Rais wetu ni mwenye kusikia kilio cha watu wake'' alisema Pinto.Kibanda na wenzake ndani ya Jukwaa la wahariri wamekuwa mstari wa mbele katika kurudisha hadhi ya tasnia ya habari na kujenga umoja miongoni mwa waandishi wa habari na kuifanya tasnia ya habari kuheshimika tofauti na ilivyokuwa nyuma.Tunaungana na kampuni ya habari, wafanayakazi wenzake, familia yake na waandishi wote kwa jumla na kumuomba Mungu amponye ili tuweze kuungana nae katika kusaidia kupasha habari Watanzania lakini ili aweze kuwaongoza waandishi wenzake.(STORI NA PICHA KWA HISANI YA BLOG YA JUMA MTANDA)
Post a Comment
Post a Comment