KAMANDA WA TAKUKURU MKOA WA MBEYA DANIEL MTUKA AKITOA MAELEZO KWA WAANDISHI WA HABARI (HAWAPO PICHANI) NAMNA AMBAVYO WALAIVYOFANIKIWA KUWANASA WALIMU WALIOKUWA WAKIWALAZIMISHA WANAFUNZI KUTOA RUSHWA YA SH. 500
SEKONDARI YA KATA YADAIWA KUFUNGUA JELA YA GUANTANAMO.
WALIMU wa shule
ya sekondari ya Forest iliyopo jijini Mbeya wamedaiwa kufungua jela maalumu
iitwayo Guantanamo inayotumika kwa ajili ya kutoa adhabu na kuwatesa wanafunzi
wnaoshindwa kutoa hongo ya sh. 500 wanapofanya makosa shuleni hapo.
Imedaiwa kuwa
wanafunzi wanapofanya makosa mbalimbali huitwa na walimu na kushinikizwa kutoa
kiasi cha sh.500 hadi 1,000, wanaposhindwa kutoa fedha hizo hupelekwa katika
chumba cha Guantnamo ambako hupewa adhabu ya kuweka kichwa chini miguu juu.
Adhabu hiyo
iliyopewa jina maarufu la 'Kuibeba Dunia' hufanyiwa wanafunzi wanaoshindwa
kutoa hongo ya fedha ambapo wale wanaotoa huachiwa huru na kuendelea na masomo.
Mara baada ya
kupatikana kwa taarifa hizo Kikosi cha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
TAKUKURU mkoani Mbeya kilituma makachero wake shuleni hapo na kukuta namna
ambavyo wanafunzi wanavyopewa adhabu ya kijeshi katika chumba cha Guantanamo.
Wakizungumza
namna ambavyo wanapewa adhabu hiyo baadhi ya wanafunzi wamesema kuwa wapo
walimu wawili maalumu kwa kutoa adhabu kwa wanafunzi ambao wameshindwa kutoa
kiasi cha sh. 500 kwa ajili ya kujikomboa.
Wamesema kuwa
walimu hao huwa na orodha ya wanafunzi wanaofanya makosa kwa siku nzima na
kuwaita mmoja mmoja na kuweka alama kwa jina la mwanafunzi aliyetoa fedha na
kwamba wale ambao wameshindwa kulipa fedha hizo hutakiwa kuingia katika chumba
cha adhabu.
Wanafunzi hao
wamebainisha kuwa wanaposhindwa kutoa kiasi cha sh. 500 hupelekwa katika jela
ambayo imepachikwa jina la Guantanamo na kupewa adhabu mbalimbali ikiwemo
kucharazwa bakora.
Kwa upande wake aliyejitambulisha
kwa jina la Sebastian Komba anayesoma kidato cha tatu shuleni hapo amesema kuwa
adhabu hiyo ameikuta tangu anaingia shuleni hapo na kwamba mara nyingi
wamekuwa wakilalamika kwa uongozi wa serikali ya shule hadi kwa Mkuu wa shule
lakini hakuna ufumbuzi unapatikana.
Naye mwanafunzi
wa kidato cha kwanza aliyejitambulisha kwa jina la Amina Moses alisema wamekuwa
wakifanyiwa unyama huo kwa muda mrefu, na kwamba yeye binafsi alimweleza mzazi
wake ambapo alisema kuwa atafuatilia kujua undani wake.
Akizungumzia
tukio hilo ofisini kwake Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mbeya Daniel Mtuka amesewataja
walimu hao ambao wamekutwa na jumla ya sh.64,000 kuwa ni Faustin Robert na
Josephat Mwasote.
|
Post a Comment
Post a Comment